Monday, October 20, 2014

JINSI YA KU-ROOT HUAWEI Y300 NA UNLOCK BOOTLOADER


Huawei Y300 ni simu nzuri ambayo inaweza kufanya mambo mengi licha ya kuwa bei nafuu. Uzuri huo wa huawei y300 huongezeka pale utakapo root simu yako na ku-unlock bootloader.

Endapo utafanikiwa ku-unlock bootloader na ku-root huawei Y300 basi utaweza kufanya yafwatayo


  1. Kuweka custom rom mbali mbali kama slimkat inayo tumia android 4.4.4
  2. Utaweza kuweka Exposed framework ambayo itakusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako
  3. Utaweza kuweka bootanimation tofauti 
Hizo ni baadhi ya faida ambazo utapa endapo uta root na ku unlock bootloader. Bila ya kuongea sana tuangalie jinsi gani utaweza ku-unlock bootloader na root huawei Y300



VIGEZO NA MASHARTI VYA KUZINGATIA KABLA UJA ROOT NA KU-UNLOCK BOOTLOADER

  1. MIMI SITAHUSIKA ENDAPO UTAARIBU SIMU YAKO
  2. HAKIKISHA UNA UWELEWA KIDOGO WA COMPUTER
  3. GENERAL COMMON SENSE IS REQUIRED
  4. WINDOW PC
JINSI YA KU UNLOCK BOOTLOADER, ROOT NA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE HUAWEI Y300

STEP 1
 Download HuaweiY300v1.1.exe        DOWNLOAD NOW.   Kisha install kwenye computer yako

STEP 2  
Baada ya ku-install program nenda kwenye local disk kisha hakikisha folder lenye jina la HuaweiY300 AIO lipo ndani ya program files na sio program files(x86). Kama lipo ndani ya
program files(x86) hakikisha unalipeleka (move) kwenye program files. Endapo hutafanya hivyo basi program yako haitafanya kazi



STEP 3
Baada ya kuliamisha folder lenye jina la HuaweiY300 AIO kwenda program files, lifungue hilo folder kisha ndani utakuta mafolder matatu. Fungua folder linaloitwa tools kisha utaona mafolder mawili. Fungua folder linaloitwa unlocktools kisha utaona mifile yafutayo



STEP 4
Double click program inayoitwa HuaweiY300 ambayo ipo ndani ya unlocktools folder na kisha click button inayoitwa Install driver ambayo ipo kushoto juu kabisa


  STEP 5
Kwenye simu yako nenda kwenye setting kisha developer options na tick kibox kinachosema USB DEBUGGING (debug mode when usb is connected)


STEP 6
Zima simu yako ya huawei y300 kisha toa battery suburi kama 5sec kisha rudisha battery halafu bonyeza na kushikilia kitufe cha kupunguza sauti (vol down) kisha bonyeza cha kuwashia (power button) huku ukiwa umeendelea kushikilia kitufe cha kupunguza kisha subiri kama 10sec huku ukiwa bado umeshikilia kitufe cha kupunguza sauti (vol down) kisha achia kitufe cha kupunguza sauti (vol down). Simu yako itaonyesha logo ya huawei lakini haitawaka. Chomeka usb cable kwenye computer na simu yako. 

STEP 7
Bonyeza Kitufe kinachosema check bootloader status(kipo upande wa kulia juu kabisa). Program yako itakuonyesha kama bootloader yako ipo locked or unlocked. Picha chini inaonyesha simu yangu ipo unlocked kwa maana tayari nimesha unlock bootloader kwenye simu yangu ya huawei y300.


STEP 8

Kama program itasema bootloader lock status : LOCKED. Bonyeza herufi yeyote kwenye computer yako na simu yako ita reboot. Au chomoa usb kisha toa battery halafu rudishia kisha washa simu yako. 
  1. kwenye simu yako piga namba hii  *#*#1357946#*#*  ili kupata product ID kisha copy hiyo namba kwenye notepad au andika sehemu
  2. kwenye simu yako nenda  (Settings -> About phone -> Status)  kisha tafuta IMEI number kisha copy hiyo namba kwenye notepad au andika sehemu
  3. Zima simu yako kisha toa battery kisha tazama  serial number S/N ya simu yako kisha copy hiyo namba kwenye notepad au andika sehemu
  4. Juu kabisa utaona sehemu wameandika model ya huawei yako. Copy hiyo model sehemu. Model ambazo zinafaa kuwa unlocked ni Y300-0151 na Y300-0100 na Y300-0000. Kama simu yako ni moja ya hizo model nilizotaja unaweza kuendelea step 9

STEP 9
Tembelea hii site http://emui.huawei.com/en/plugin.php?id=unlock&mod=detail
kisha utaona  unatakiwa ujiandikishe kwanza ndipo utakapoweza kupata form kama picha inavyo onekana chini.



  

Jaza viboksi vyote kisha bonyeza button inayosema submit ambayo ipo kwa rangi nyekundu. Baada ya kubonyeza submit chini kabisa utaona umepewa unlock code ya simu yako na itakuwa imeandikwa kwa rangi nyekundu. Copy hiyo unlock code sehemu kwa maana utaitaji kwenye step 10

STEP 10
 Rudia kama ulivyofanya kwenye STEP 6. Kwenya program yako bonyeza button inayosema 1 Unlock bootloader. Kisha andika ile unlock na bonyeza inter. utaona picha inayofanana na hii. 



 Press enter au any key kwenye computer yako ili uweze ku unlock bootloader. Baada ya hapo utakuwa umefanikiwa ku unlock bootloader ya simu yako ya huawei y300.

STEP 11
Kipengele hichi ni kama unapenda kuweka custom recovery kwenye huawei yako. Custom recovery ni njia moja muhimu inayokuwezesha kuweka custom rom kwenye simu yako.
Kama unataka kuweka custom recovery  hakikisha unazima simu yako. Rudia step 6.

 Kwenye program yako bonyeza button inayosema 2 install recovery na utaona picha kama inavyoonekana chini

 Press enter mara mbili au key yoyote mara mbili kwenye computer yako ili uweze kuweka custom recovery. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako. Kuakikisha kama umefanikiwa kuweka custom recovery unatakiwa uzime simu yako kisha bonyeza cha kuwashia pamoja na cha kuongezea sauti kwa pamoja na vishikilie mpaka utakapoona display yako inaonyesha kama picha chini


Mpako hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako. Bonyeza kipengele cha reboot na simu yako itawaka kama kawaida.

STEP 12
Kipengele hichi ndio cha mwisho na kinaelezea jinsi ya ku root huawei.  Kwenye program yako bonyeza button inayosema 3 super user(Root) kisha itafunguka new window ambalo ndani yake kuna file linaitwa SuperSU-v1.86. Copy hilo file kwenye memory card ya simu yako. Kisha zima simu yako na tazama video chini jinsi ya kuendelea.


Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa ku-root huawei y300. Endapo umeshindwa kufwata maelekezo niliyoyatoa hapo juu basi unaweza wasiliana nasi na utasaidiwa kwa gharama isiyopungua Tsh 25,000. Piga hii namba +255753877552. 

Kama una swali, please  drop your comment below. Please don't forget to like our facebook page and subscribe to our youtube channel. Thanks
 

7 comments:

  1. step 9; link inaandika forbidden. msaada plz

    ReplyDelete
  2. kaka link inasema forbidden.. help me please

    ReplyDelete
  3. unlock code ya huawei kwa sasa inapatikana hapa
    http://emui.huawei.com/en/plugin.php?id=unlock&mod=detail
    unatakiwa kwanza ujiandikishe kwenye website kisha ndio utaweza kupata form ya kujaza ili upate unlock code

    ReplyDelete
  4. please bro the link download now of huawei y300 aio is invalid please help me

    ReplyDelete
    Replies
    1. https://www.dropbox.com/s/l0mkwj1i3y5r5hh/HuaweiY300%20AIO.zip?dl=0

      Delete