Tuesday, March 22, 2016

DOWNLOAD MIITO(RINGTONES) YA SAMSUNG GALAXY S7

Kama wewe ni mpenzi wa simu za samsung na ungependa na wewe utumie miito(ringtones) iliyopo kwenye Samsung Galaxy S7 basi utakuwa haujachelewa. Sasa unaweza download miito iliyopo kwenye Samsung Galaxy S7 na uanze kuitumia kwenye simu yako ya android.

Tumia link chini ili uweze kudownload miito ya Samsung Galaxy S7.
http://downloadmirror.co/android/SLb/s7tones.zip

Baada ya kumaliza ku-download, extract file ulilo download kwa kutumia program kama 7zip, winRar na ndani yake utakutana na mafolder matatu ambayo ni Notification, Ringtones, ui.

Kama wewe ni mtaalamu zaidi kwenye maswala ya android basi unaweza ukayapangilia vizuri mafile hayo kwenye simu yako. Ili kuweza kuyapangilia mafile hayo matatu kwenye simu yako fwatilizia maelekezo chini na hakikisha simu yako ipo rooted

JINSI YA KUIWEKA MIITO YA SAMSUNG GALAXY S7 KWENYE SIMU YAKO

STEP 0

Cha kwanza unatakiwa ujue ringtones pamoja na notifications huwa zinakaa wapi kwenye simu yako. Kwa kutumia Es File Explorer nenda kwenye Device kisha System halafu tafuta folder linaloitwa media kama picha inavyo onekana chini.

STEP 1

Ndani ya Folder la Media utakutana na folder linaloitwa audio. Ndani ya folder la audio utakutana na mafolder yenye majina kama Notification, Ringtones, ui. Tazama picha chini kuelewa zaidi.

STEP 2

Una kumbuka lile file lenye miito ya Samsung Galaxy S7 ulilo donwload mapema? Ndani yake ulikutana na mafolder yenye majina kama yaliyopo kwenye folder la audio ambalo umelifungua kwenye Step 1.

STEP 3

Sasa anza kuamisha mlio mmoja mmoja kutoka kwenye lile file ulilo download na upeleke kwenye folder ambalo linaendana na ambalo lipo kwenye simu. Mfano kama umetoa mlio kutoka kwenye folder la ringtone basi hakikisha unalipeleka kwenye folder la ringtone ambalo lipo kwenye simu yako.

STEP 4

Baada ya kupeleka au ku copy mlio kwenye simu yako ukiwa unatumia Es File explorer, shikilia mlio ambao umeupeleka mpaka utakapoona umepata alama ya tick kisha bonyeza vidoti vitatu juu kulia na bonyeza kipengele kinachoitwa properties halafu shuka chini hadi kwenye kipengele kilicho andikwa permission halafu bonyeza sehemu iliyo andikwa change na weka tick sehemu ambazo nimeweka kama picha inavyo onekana chini. Hakikisha tick zako zinafanana na picha chini. Endapo hutafanya hivyo basi huo mlio hautafanya kazi kwenye simu yako



Rudia Step 4 kwa kila muito ambao utaupeleka kwenye simu yako. Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram kwa kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment