Monday, March 21, 2016

INSTAGRAM WAMERUHUSU KUTUMIA ACCOUNT ZAIDI MOJA KWENYE SIMU ZA ANDROID

Kama wewe ni mtumiaji wa Instagram na umekuwa na account mbili tofauti sasa unaweza kuzitumia account hizo mbili kwa wakati mmoja kwenye simu yako ya android. Hata kama una account zaidi ya mbili bado utaweza kuzitumia zote kwenye simu yako ya android.

Ili kuweza kutumia account zaidi ya moja kwenye simu yako unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye seeting za instagram halafu chini kabisa utaona kipengele kinachosema add account kama picha inavyo onekana chini.



Endapo utafanikiwa kuongeza account yako nyingine na ungependa kuhama kutoka kwenye account moja kwenda nyingine basi nenda kwenye page yako ya instagram kisha tazama juu kushoto pale kwenye username utaona kimshale kinaelekea chini. Bonyeza kisha utaona account zako na utaweza kuchagua ipi unataka iwe active. Tazama picha chini kuelewa zaidi.



Mpaka hapo utakuwa umeweza kutumia account zaidi ya moja za instagram kwenye simu yako ya android. Kama umependa kazi zetu unaweza ukatufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment