Friday, July 8, 2016

JINSI YA KUWEKA AU KUBADILISHA IMEI KWENYE SIMU ZA ANDROID

Imei ni kitu cha msingi sana kwenye simu yako maana ndio inakusaidia wewe kuweza kupata mawasiliano. Endapo simu yako itapoteza Imei zake basi utajikuta simu yako haiwezi kupata mawasiliano yeyote.

Leo tutajifunza njia itakayo kusaidia kuweka Imei kwenye zile simu ambazo zimepoteza Imei. Njia hii imeajaribiwa kwenye simu ya android (Tecno H6). Njia hii inafanya kazi kwenye simu zote zinazotumia MTK (MediaTek Processor).

Tahadhari

USITUMIE HII NJIA KUBADILISHA IMEI KWENYE SIMU AMBAZO ZIMEFUNGIWA KUTOKANA NI FAKE, UTAFUNGWA. MIMI SITAHUSIKIA ENDAPO UTAVUNJA SHERIA ZA TCRA TANZANIA. TUMIA HII NJIA KUJIFUNZA NA SIO KUVUNJA SHERIA.

STEP 0

Hakikisha simu yaki tayari imekuwa rooted. Kwa wale ambao hawana uwakika kama simu zao zipo rooted unaweza tembelea link chini kujua kama simu yako ipo rooted.
https://phonetricktz.blogspot.com/2014/11/jinsi-ya-kujua-kama-simu-yako-imekuwa.html

STEP 1

Download Mtk Engineering mode kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu yako.
https://www.dropbox.com/s/cgeppq446ebofks/MTKEngineerMode_v1.1.1.apk?dl=0

STEP 2

Fungua Mtk Engineering mode kwenye simu yako. Utapata muonekano kama picha chini

STEP 3

Bonyeza kipengele kinachosema MTK Engineer Mode na utapata muonekano kama picha chini

STEP 4

Nenda kwenye kipengele cha connectivity kama picha chini

STEP 5

Bonyeza kipengele kilicho andikwa CDS Information na utapata muonekano kama picha chini

STEP 6

Bonyeza kipengele kilicho andikwa Radio Information na utapata muonekano kama picha chini


Note

Endapo simu yako itaonyesha phone 1 na phone 2 basi simu yako inatumia line mbili na utatakiwa kuweka Imei mbili tofauti ili simu yako iweze kusoma network

STEP 6

Bonyeza kipengele kilicho andikwa Phone 1 na utapata muonekano kama picha chini

STEP 6

Juu kabisa utaona sehemu imeandikwa AT+. Tap au bonyeza mbele ya alama ya jumlisha kisha ruka nafasi moja na kisha andika maneno yafuatayo bila kukosea.. AT+ EGMR=1,7,”IMEI Number unayotaka kuweka” mfano mimi nataka kuweka imei number 34226718292020 basi itakuwa hivi AT+ EGMR=1,7,”34226718292020". kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa SEND AT COMMAND

Kwa wale ambao watabonyeza Phone 2 basi wanatakiwa kuandika hivi AT+ EGMR=1,7,”IMEI Number unayotaka kuweka” mfano mimi nataka kuweka imei number 34226718292020 basi itakuwa hivi AT+ EGMR=1,7,”34226718292020". kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa SEND AT COMMAND. Tazama picha chini kuelewa zaidi.

STEP 6

Zima na kuwasha simu yako. Kisha piga number *#06# kuhakikisha Imei number uliyoweka

Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz au wasiliana nasi kupitia whatsapp +255627732383.

2 comments: