Sunday, August 7, 2016

GALAXY NOTE 7, KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA

Samsung Galaxy Note 7 ni toleo jipya kutoka Samsung ukiachana na Samsung Galaxy S7 Edge. Galaxy Note 7 imekuja na mambo mengi mapya ambayo hayakuwepo kwenye simu ya aina yoyote ambayo imeshawai kutengenezwa na Samsung. Kwanza kabisa hii simu imepewa Slogan inayosema "The smartphone that thinks big"

Gorilla Glass 5

Samsung Galaxy Note 7 ndio simu ya kwanza kuwa na kioo ambacho kinachoitwa Gorilla Glass 5 ambacho ni imara sana na kinaweza kustahimili kishindo kutoka urefu wa futi tano(5FT) bila kupasuka au kupata mchubuko wa aina yeyote.

Iris Scanner

Galaxy Note 7 imekuja na mfumo mpya kabisa ujulikanao kama Iris Scanner. Kama ilivyozoeleka simu za Android kuweza kusoma alama ya vidole basi Samsung wame endelea mbele kidogo na sasa wanaweza kukutambua wewe kwa kutumia macho yako. Hii ina maanisha simu yako itakuwa haiwezi kuingilika ovyo ovyo maana Samsung wameboresha ulinzi kwenye Galaxy Note 7. Wale wenzetu wa Note 4 na Note 3 msiwaze sanaa ipo siku tu...

Storage

Kwa wale wanaopenda simu yenye uwezo wa kuhifadhi vitu vingi basi Galaxy Note 7 ndio JIBU. Note 7 inakuja na ukubwa wa 64GB kama memory ya simu na pia ina sehemu ya kuweka memory card yenye ukubwa hadi kufikia 256GB.....

Usb Type C

Samsung wameamua kutumia mfumo mpya wa usb ambao unajulikana kama Usb Type C. Kiukweli hapa Samsung amechelewa sana kufanya haya mabadiliko maana simu nying tayari zilikuwa zimeshaanza kutumia Usb Type C. Unaweza jiuliza Usb Type C ni nini? Cha kwanza unachotakiwa kugundua ni kwamba kabla ya Usb Type C tulikuwa tunatumia Usb Type A. Usb Type C ni ndogo zaidi ya Usb Type A na ina uwezo mkubwa wa kutuma na kupokea vitu kushinda Usb Type A..

Water Resistant

Kama ilivyo kwenye Galaxy S7 Edge, Galaxy Note 7 haingii maji na unaweza kuitumia hata ukiwa bafuni, kwenye mvua kwenye Swimming Pool yaani ushindwe wewe tu. Sio simu tu ambayo ni Water Resistant hata S Pen nayo ni water resistant...

System

Kwenye upande wa System, Galaxy Note 7 inatumia Android 6 (Marshmallow) na pia imekuja na kitu kipya kinachoitwa GraceUX. Wengi wetu tunatumia Touchwiz Interface lakin Galaxy Note 7 imekuja na interface mpya kabisa ambayo imepewa jina la GraceUX. Kiukweli GraceUX ina muonekano mzuri kushinda Touchwiz.

Hardware

Galaxy Note 7 inakuja na Ram ya 4GB na Kioo chenye ukubwa wa 5.7 Inch Quad AMOLED na processor ya Quad-core 2.3 GHz Mongoose + quad-core 1.6 GHz Cortex-A53 ikiwa na Camera ya nyuma yenye 12 Megapixels na Camera ya mbele yenye 5 Megapixel pamoja na Battery ambayo haitoki yenye ukubwa wa 3500 mAh .

Tazama video fupi chini ikiwa inaonyesha muonekano wa Galaxy Note 7


Mwisho kabisa Samsung wameiruka Galaxy Note 6 ili wapate muendelezo ambao utakuwa unakwenda sambamba na Galaxy S series.. S7 na Note 7..na Sio S7 na Note 6.

No comments:

Post a Comment