Showing posts with label samsung. Show all posts
Showing posts with label samsung. Show all posts

Friday, January 9, 2015

JINSI YA KUJUA KAMA SIMU YA SAMSUNG NI ORGINAL AU FAKE



Wengi wetu tumekuwa tukishindwa kutofautisha kati ya orginal na fake samsung mobile device.

Wengi wamekuwa wakijikuta wananunua simu fake tena kwa gharama kubwa. Hizi ni baadhi ya njia ambazo zitakuwezesha kuitambua simu orginal ya samsung

Saturday, December 20, 2014

MUONEKANO WA ANDROID 5.0 (LOLLIPOP) KWENYE SAMSUNG GALAXY S3


Ni meizi kadhaa imepita tangu google watangaze android 5.0 ambayo ndio itakuwa baba wa android kitkat. Wengi wamekuwa wakisubiria android 5.0 ili kuona muonekano wake.

Android 5.0 imeongezwa vitu vingi ukilinganisha na android 4.4.4. Baadhi ya vitu vilivyoongezwa ni screen pinning, battery saver, system animation, user account, device encryption na mengine mengi.

Monday, November 3, 2014

(VIDEO) SAMSUNG GALAXY S3 IKIWA NA MUONEKANO WA NOTE 4


Samsung Galaxy S3 GT-I9300 imeweza kupata muonekano wa Note 4. Muonekano mzima wa Note 4 pamoja na application nyingi zilizopo kwenye Note zimeingizwa kwenye Samsung Galaxy S3.
Kwa kifupi simu yangu ya S3 imekuwa kama Note 4.

Tazama video chini ikionyesha jinsi Samsung Galaxy S3 ikiwa na muonekano wa Note 4

Thursday, October 23, 2014

JINSI YA KUBADILI SAMSUNG GALAXY S3 KUWA KAMA SAMSUNG GALAXY S4


Kama wewe unatumia simu aina ya Samsung Galaxy S3 GT-I9300 na umekuwa ukitamani sana utumie Samsung Galaxy S4. Napenda kukwambia kwamba sasa unaweza badilisha muonekano mzima wa Samsung Galaxy S3 na kupata muonekano wa S4.

Kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba Samsung Galaxy S3 tayari ipo rooted. Kama bado uja root Samsung Galaxy S3 tembelea hii link http://phonetricktz.blogspot.com/2014/07/maelekezo-root-samsung-galaxy-s3-gt.html

Kitu cha pili unachotakiwa kufanya baada ya kuroot simu yako ni kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S3. Kama bado ujaweka custom recovery tembelea hii link http://phonetricktz.blogspot.com/2014/06/maelekezo-weka-custom-recovery-kwenye.html

Baada ya Kumaliza ku-root na kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S3, unaweza sasa badili muonekano mzima wa Samsung Galaxy S3 na upate muonekano wa S4.

Thursday, July 31, 2014

(MAELEKEZO) ROOT SAMSUNG GALAXY S3 GT-I9300


Samsung Galaxy S3 ni moja ya simu kali sana na bado bei yake ni kubwa licha ya kuwa ni toleo la kizamani. Endapo kama ungependa uendelee kuifurahia samsung galaxy s3 huna budi kuifanyia rooting ili uweze kutumia vitu kama exposed framework au hata kuweka custom rom.

Sasa leo ntatoa maelekezo mafupi ambayo yatakuwezesha ku root SAMSUNG GALAXY S3 GT-I9300 . Endapo utafanikiwa ku root simu yako basi utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutumia custom rom na hata Exposed Framework.

Kabla sijatoa maelekezo ni vyema nikupe masharti ambayo unatakiwa kukubaliana nayo kabla uja root simu yako

Monday, July 28, 2014

(MAELEKEZO) ROOT SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100


Root ni kitu muhimu sana kwenye simu zinazo tumia mfumo wa android. Bila ku root simu yako hautaweza kufurahia simu yako. Kitu kizuri kuhusu android ni uwezo wa kuibadilisha na kuongeza vitu vizuri kwenye simu yako.

Sasa leo ntatoa maelekezo mafupi ambayo yatakuwezesha ku root SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100. Endapo utafanikiwa ku root simu yako basi utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutumia custom rom na hata Exposed Framework.

Kabla sijatoa maelekezo ni vyema nikupe masharti ambayo unatakiwa kukubaliana nayo kabla uja root simu yako

Friday, July 25, 2014

(MAELEKEZO) JINSI YA KU-ROOT SAMSUNG GALAXY S DUOS GT-S7562


Hii ni njia rahisi itakayo kuwezesha ku root simu aina ya Samsung Galaxy S Duos GT-S7562. Moja ya faida ya kuroot simu ni kuweza kubadili muonekano wa simu yako pia utaweza kuweka custom rom au kuweka exposed framework kwenye simu yako.

Leo nitatoa malekezo ambayo yatakusaidia endapo ungependa ku root Samsung Galaxy S Duos GT-S7562. Kabla sijatoa maelekezo ni vyema nikupe masharti ambayo unatakiwa kukubaliana nayo kabla uja root simu yako

Tuesday, July 15, 2014

(MAELEKEZO) JINSI YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY NOTE 2 IPATE MUONEKANO WA SAMSUNG GALAXY NOTE 3


Kwa wale wenye Samsung galaxy note 2 GT- N7100 sasa wanaweza kuzigeuza simu zao na kupata muonekano wa kisasa wa Samsung Galaxy Note 3. Hii inamaanisha utakuwa unatumia apps za samsung ambazo zipo kwenye galaxy note 3 na Samsung Galaxy S5.

Baadhi ya apps ambazo utazipata kwenye Note 2 ni
  • S5 Toolbox feature
  • S5 Power Saving Mode
  • S5 Ultra Power Saving Mode
  • S5 Lockscreen Effects
  • S5 System UI
  • S5 Launcher with Magazine & Pullup app
  • S5 Wallpaper
  • Note 3 Icons
  • Note 3 MyFiles
  • Note 3 SNote
  • Note 3 ScrapBook
  • Note 3 SketchBook
Tazama video ikionyesha Samsung Galaxy Note 2 GT N7100 ikiwa na muonekano wa Galaxy Note 3.

Monday, July 14, 2014

(MAELEKEZO) JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY NOTE 2 GT-N7100



Leo tutazungumzia jinsi ya kuweka Custom Recovery kwenye Samsung Galaxy Note 2 GT-N7100. Kwa kifupi hautaweza kutumia Custom Rom kama hauna Custom Recovery kwenye simu yako.

Sasa kama wewe ungependa kutumia Custom Rom kwenye Samsung Galaxy Note 2 GT-N7100 huna budi kuweka custom recovery kwenye note 2. Aina ya custom recovery tutakayoweka kwenye Samsung Galaxy Note 2 GT-N7100 ni philz touch recovery.

Kujua aina ya recovery ambayo imekuja na samsung note 2 GT-N7100 unatakiwa kuizima simu yako kisha Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano na utaona recovery ambayo huwa inakuja na simu yako. Sasa sisi tunachofanya ni kuitoa hiyo iliyokuja na simu na kuweka PHILZ TOUCH RECOVERY. ambayo ina uwezo mkubwa.



Kabla sijatoa malekezo jinsi ya kuweka Philz Touch Recovery kwenye Samsung Galaxy Note 2 GT-N7100 ni vyema kukupa vigezo vya kuzingatia kabla ujajaribu kuweka custom recovery.

Monday, July 7, 2014

(MAELEKEZO) JINSI YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY S4 IPATE MUONEKANO WA S5



Hi ni habari njema kwa wale wanaotumia Samsung Galaxy S4 GT-I9500. Wale wanaotumia Samsung Galaxy S4 GT-I9500 usikubali hi habari ikupite hivi hivi bila kujaribu kwenye simu yako.

Kupitia Revosoft Rom utaweza kutumia apps za S5 kama Samsung Health na nyinginezo nyingi na pia utapata ule muonekano wa S5 kwenye S4 yako. Baadhi ya picha zikionyesha Samsung Galaxy S4 ikwa na muonekano wa S5 na ikiwa inatumia baadhi ya apps za S5.


Sunday, July 6, 2014

(MAELEKEZO) JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S4.


Kwa wale wanaopenda ku-flash simu zao na kuzipa muonekano wa ukweli basi watakuwa wameshasikia kuhusiana na custom recovery. Custom Recovery ni njia ambayo itakuwezesha kutumia custom rom kwenye simu.

Leo tutaongelea jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S4 (GT-I9500).
Jina la custom recovery ambayo tutaweka kwenye S4 (GT-I9500) ni PHILZ TOUCH RECOVERY.

Kujua aina ya recovery ambayo imekuja na samsung galaxy S4 unatakiwa kuizima simu yako kisha Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano na utaona recovery ambayo huwa inakuja na simu yako. Sasa sisi tunachofanya ni kuitoa hiyo iliyokuja na simu na kuweka PHILZ TOUCH RECOVERY. ambayo ina uwezo mkubwa 


Kabla sijatoa malekezo jinsi ya kuweka Philz Touch Recovery kwenye S4 (GT-I9500) ni vyema kukupa vigezo vya kuzingatia kabla ujajaribu kuweka custom recovery kwenye S4.

Wednesday, July 2, 2014

(MALEKEZO) IFANYE SAMSUNG GALAXY S3 I9300 KUWA KAMA S5


Leo tutaangalia jinsi ya kuifanya Samsung Galaxy S3 I9300 ipate muonekano wa S5 pia iweze kutumia apps za S5. Custom Rom ambayo tutatumia inaitwa Galaxy S5 mini.

Watu wengi sana wanaotumia simu za android huwa hawajua kama unaweza ukaweka custom rom kwenye simu ya android. Unaponunua simu ya android kama Samsung ndani yake kuna stock rom. Navyosema stock rom namaanisha kama computer zinavyokuja na window os.

Kitu kizuri ni kwamba watumiaji wa simu wanaweza wakabadilisha kutoka kwenye stock rom na kutumia custom rom. Custom rom hizi ni rom ambazo zimeongezewa maujanja ili kukupa muonekano mzuri wa simu yako na pia kuongeza ufanisi kwenye simu yako.

Tusiongee sana, angalia picha zikionyesha Samsung Galaxy S3 ikiwa inamuonekano wa S5 na ikitumia apps nyingi za S5.

Sunday, June 29, 2014

(MAELEKEZO) WEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S3 I9300, I9305


Custom Recovery ni njia kuu inayo kuwezesha wewe mtumiaji wa Samsung Galaxy S3 I9300 au I9305 kuweza ku-flash rom tofauti tofauti kwenye simu yako. Kwa kifupi hautaweza kutumia Custom Rom kama hauna Custom Recovery kwenye simu yako

Leo nitatoa maelekezo jinsi ya kuweka custom recovery (PHILZ TOUCH RECOVERY) kwenye Samsung Galaxy S3 I9300. Hakikisha unasoma malekezo yote halafu ndio ujaribu kwenye simu yako.


Sunday, June 22, 2014

(MALEKEZO) JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100.


Watu wengi wanaotumia simu za android bado hawajaweza kuzitumia simu zao kwa asilimia mia moja. Kwa wale wanaotumia SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100 leo nitawaonyesha njia ya kuweza kutumia simu zao zaidi kushinda wanavyotumia kwa sasa.

Leo nitatoa maelekezo jinsi ya kuweka custom recovery kwenye SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100. Kuna aina nyingi za custom recovery lakini mimi nitaiongelea PHILZ TOUCH RECOVERY. 



Faida moja kubwa ya kuweka custom recovery kwenye simu yako ni kuweza ku-flash ROM tofauti tofauti na kuongeza ufanisi kwenye simu yako. Zipo faida nyingi sana. Ukitaka kujua faida nyingine basi wewe check google.

Bila kuongea sana, tupate maelekezo jinsi ya kuweka custom recovery kwenye SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100

Sunday, June 15, 2014

IFANYE SAMSUNG GALAXY NOTE 2 IWE KAMA GALAXY NOTE 3



Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa Samsung Galaxy Note II GT-N7100, N7105 basi unaweza ukaibadilisha simu yako na kupata muonekano wa Samsung Galaxy Note 3.

Kupitia DN3 (Ditto Note 3) ROM itakuwezesha kuifanya Samsung Galaxy Note II GT-N7100, N7105 kupata muonekano wa Samsung Galaxy Note 3.

Kabla uja flash hii rom unatakiwa uwe na custom recovery kwenye simu ambayo itakuweza kufanya backup na kuflash  DN3 (Ditto Note 3) ROM. Bila custom recovery itakuwa ni ndoto kuifanya Samsung Galaxy Note II iwe kama Galaxy note 3

Maelekezo ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy Note 2 yanapatikana HAPA

Kama tayari unayo custom recovery kwenye Samsung Galaxy Note II basi unaweza kuendelea na kuifanya Samsung Galaxy Note II iwe kama samsung galaxy note 3.

Baadhi ya picha zikionyesha Samsung Galaxy Note 2 ikiwa na muonekano wa Samsung Galaxy Note 3

Thursday, June 12, 2014

(MAELEKEZO) JINSI YA KUINGIA KWENYE RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S3 NA SIMU NYINGINE ZA SAMSUNG


Wale ambao hawajui nini maana ya recovery mode basi leo nitatoa maelezo kidogo kuhusiana na recovery mode.

Simu nyingi zinazotumia mfumo wa android huwa zinakuwa na recovery mode. Kama jina livyosema "Recovery" hii ni sehemu muhimu sana kwenye simu yako na inakupa uwezo wa kurekebisha simu yako endapo itakuwa inakupa matatizo madogo madogo.

Kwa mfano, Samsung Galaxy S3 inakuja na recovery na jinsi ya kuingia kwenye recovery kwenye Samsung galaxy s3 ni rahisi sanaa. Kuingia kwenye recovery mode haiwezi kuleta madhara yoyote kwenye simu yako bali utakuwa umeijua simu yako kiundani zaidi.

JINSI YA KUINGIA KWENYE RECOVERY KWA WALE WANATUMIA SAMSUNG GALAXY S3 NA SIMU NYINGINE ZA SAMSUNG

Thursday, May 29, 2014

JINSI YA KUONDOA TATIZO LA " NOT ENOUGH SPACE" KWENYE SAMSUNG GALAXY SII I9100


Kama wewe unatumia samsung galaxy s2 i9100 na umekuwa ukipata tatizo la "not enough storage" ukiwa unajaribu kuweka apps mpya kwenye simu yako basi tatizo ni rahisi kutatulika.
.
Kwa kifupi Samsung Galaxy S2 ina ukubwa wa 16GB lakini katika hizo 16GB kuna 14GB ambazo zipo free. Ndani ya hizo 14GB zimegawanyika mara mbili. Kuna Device memory na USB storage.

Sasa ukiwa unaweka apps mpya huwa zinatumia hiyo nafasi ya Device Storage ambayo huwa na 2GB. Endapo utaweza kujaza hiyo 2GB basi utakuwa uwezi tena kuweka apps na utakuwa unapata hii error "not enough storage" kila ukiwa unajaribu kuweka au ku-update apps