Sunday, July 6, 2014
(MAELEKEZO) JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S4.
Kwa wale wanaopenda ku-flash simu zao na kuzipa muonekano wa ukweli basi watakuwa wameshasikia kuhusiana na custom recovery. Custom Recovery ni njia ambayo itakuwezesha kutumia custom rom kwenye simu.
Leo tutaongelea jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S4 (GT-I9500).
Jina la custom recovery ambayo tutaweka kwenye S4 (GT-I9500) ni PHILZ TOUCH RECOVERY.
Kujua aina ya recovery ambayo imekuja na samsung galaxy S4 unatakiwa kuizima simu yako kisha Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano na utaona recovery ambayo huwa inakuja na simu yako. Sasa sisi tunachofanya ni kuitoa hiyo iliyokuja na simu na kuweka PHILZ TOUCH RECOVERY. ambayo ina uwezo mkubwa
Kabla sijatoa malekezo jinsi ya kuweka Philz Touch Recovery kwenye S4 (GT-I9500) ni vyema kukupa vigezo vya kuzingatia kabla ujajaribu kuweka custom recovery kwenye S4.
(VIGEZO NA MASHARTI)
1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S4 (GT-I9500).
4: You need common sense and brain.
5: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window
6: Install Samsung kies kwenye compuer yako ili kupata drivers za samsung galaxy S4. Samsung Kies inapatikana HAPA. Hakikisha unadownload kies na sio kies3
MAELEKEZO YA KUWEKA PHILZ TOUCH RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S4 GT-I9500
STEP 0
Hakikisha kama simu yako ni model GT-I9500. Kama ni tofauti na hiyo tafadhali usiendelee unaweza ukaharibu simu yako.
STEP 1
Download Odin program zip file kwenye computer yako DOWNLOAD
Jina la file ni Odin3 v3.09.zip
STEP 2
Download Philz Touch Tar file kwenye computer yako DOWNLOAD
Hakikisha jina la file utakalo download ni philz_touch_6.41.6-i9500.tar.md5
Likimaliza kujidownload likopi na uliweke kwenye desktop ya computer yako
STEP 3
Unakumbuka lile file ulilo-download kwenye step1 (Odin zip file, Odin3 v3.09.zip)? sasa lifungue (Extract/Unzip) kwenye computer yako kwa kutumia (7-zip free software, au Win Rar) ili upate hili file. Odin3 v3.09.exe kisha liweke kwenye desktop pamoja na lile file ambalo umelidownload kwenye step 2 ambalo ni philz_touch_6.41.6-i9500.tar.md5
STEP 4
Double-click the Odin3 v3.09.exe file to open Odin
STEP 5
Izime simu yako kisha subiri kama sekunde 10.Washa simu yako ya samsung galaxy S4 kwenye download mode. Tazama picha chini kisha soma maelekezo chini ya picha kujua jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode
Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode bonyeza kitufe cha katikati (Home) + cha kupunguza sauti (Volume down) + na cha kuwashia (power) kisha vishikilie kwa pamoja mpaka utakapoana kwenye screen yako maneno yanayosema Press Volume Up now to continue to Download Mode. Sasa achia halafu bonyeza cha kuongeza sauti. (Volume up)
Hakikisha simu yako inamuonako kama picha ya kulia inavyoonyesha chini kabla ujaendele kwenye step 6.
STEP 6
Kwenye computer yako hakikisha uko kwenye ile Odin program ambayo uli double click kwenye step 4. Sasa chomeka simu kwenye computer ikiwa bado kwenye download mode kwakutumia usb cable. Odin itaitambua simu yako na itaonyesha message kama inavyoonekana kwenye picha chini
STEP 7
Kwenye Odin Click AP button na chagua lile file ambalo uli download kwenye step 2 ambalo uliliweka kwenye desktop. Jina la file ni philz_touch_6.41.6-i9500.tar.md5
Muekano wako kwenye computer utakuwa hivi endapo utakuwa umenifwatilia vizuri. Tafadhali naomba Odin yako kwenye computer iwe na muonekano kama huo. Viboksi ambavyo vinatakiwa viwe na alama ya vema ni Auto Reboot na F.Reset Time kama inavyoonekana kwenye picha.
STEP 8
Kabla ya kuendelea hakikisha tupo pamoja. Usiendele kama ujaelewa.
STEP 9
Kwenye Odin bonyeza start button ambayo ipo chini kabisa kisha subiri mpaka utakapoana Odin imekuandikia PASS kama picha inavyoonyesha chini. Chomoa simu yako kwenye computer kisha subiri mpaka itakapowaka yenyewe kama ikichelewa kuwaka basi bonyeza cha kuwashia na itawaka kama kawaida.
STEP 10
Hongera mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako ya galaxy S4 (GT-I9500) na utakuwa na uwezo wa kuflash rom mbalimbali ili kupata muonekano mzuri na kuongeza ufanisi zaidi.
Ili kuhakikisha simu yako ina custom recovery basi zima simu yako kisha subiri kama sekunde kumi. Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano. Endapo utafanikiwa basi simu yako itakuwa na muonekano ambao unafana na picha inavyoonyesha chini.
Endapo kama wewe ungependa uweke custom recovery kwenye simu yako na hauwezi basi wasiliana nasi kupitia namba +255753618318 au +255716203029 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000.
Kama una swali toa maoni (comment) chini hapo na utajibiwa. Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
Labels:
samsung
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment