Monday, July 7, 2014
(MAELEKEZO) JINSI YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY S4 IPATE MUONEKANO WA S5
Hi ni habari njema kwa wale wanaotumia Samsung Galaxy S4 GT-I9500. Wale wanaotumia Samsung Galaxy S4 GT-I9500 usikubali hi habari ikupite hivi hivi bila kujaribu kwenye simu yako.
Kupitia Revosoft Rom utaweza kutumia apps za S5 kama Samsung Health na nyinginezo nyingi na pia utapata ule muonekano wa S5 kwenye S4 yako. Baadhi ya picha zikionyesha Samsung Galaxy S4 ikwa na muonekano wa S5 na ikiwa inatumia baadhi ya apps za S5.
Bila kuongea maneno mengi tuzungumzie kwanza vitu vya kuzingatia kabla ujajaribu hu ujanja kwenye Samsung Galaxy S4 yako
REQUIREMENTS ( VIGEZO VYA KUZINGATIA)
1: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy S4 GT-I9500 na sio vinginevyo.
2: Hakikisha una custom recovery kama Philz touch recovery kwenye Samsung Galaxy S4 GT-I9500. Kama wewe hujui ni maana ya Custom Recovery na ungependa kuiweka kwenye S4 yako basi tembelea hii link BONYEZA HAPA.
3: Unaelewa English japokuwa nitajitahidi kupunguza kutumia lugha ya kingereza kadri niwezavyo.
4: Hakikisha simu yako ina charge ya kutosha. Mapendekezo yangu simu yako iwe na charge kwanzia 70% na kuendelea
5: Hakikisha Memory Card yako ina nafasi isiyopungua 2GB.
6: You need common sense and brain
NOTE : MIMI SITAUSIKA ENDAPO UTAHARIBU SIMU YAKO. CONTINUE ON YOUR OWN RISK
MAELEKEZO YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY S4 GT-9500 IWE KAMA S5
STEP 0
Hakikisha kama simu yako ni model GT-I9500. Kama ni tofauti na hiyo tafadhali usiendelee unaweza ukaharibu simu yako.
STEP 1
Download Revosoft Rom HAPA kisha baada ya kumaliza kudownload liweke hilo file kwenye memory card ya simu yako. Naomba hilo file usilifungue, liweke kama lilivyo.
Jina la file ni Revosoft Project X Rom v2.5.zip Ukubwa wa file ni 1.5GB.
STEP 2
Zima simu yako kisha subiri kama sekunde 10. Washa simu yako kwenye Recovery Mode. Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye recovery mode unatkiwa ufanye hivi (Simu yako ikiwa tayari umeizima Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano na utaona recovery)
Note: tumia kitufe cha kuongeza sauti na cha kupunguza sauti kupanda na kushuka kwenye menu na bonyeza kitufe cha kuwashia kuchagua menu
STEP 3
Ukiwa bado kwenye Recovery fanya backup(nandroid backup) ya simu yako kwa kwenda kwenye kipengele cha backup and restore kisha backup
Note: backup itachukua muda kidogo hakikisha unasubiri mpaka simu yako itakapomaliza kubackup. Backup itakusaidia kurudisha simu yako kama ilivyokuwa endapo utataka kurudisha simu yako kwenye hali yake ya mwanzoni.
STEP 4
Baada ya kumaliza Ku-backup na simu yako ikiwa bado kwenye recovery mode nenda kipengele cha Wipe data/Factory reset kisha chagua YES.
Note: Kufanya Wipe data/Factory reset ni muhimu sana kuhakikisha simu yako haipati matatizo kama bootloop
STEP 4
Baada ya kumaliza ku-wipe/factory reset, nenda kwenye kipingele cha install zip kwenye recovery kisha chagua install zip from SD CARD halafu nenda kachague lile file ambalo ulidownload kwenye step 1 na kuliweka kwenye memory card yako. Hakikisha jina la file ni Revosoft Project X Rom v2.5.zip
STEP 5
Fwatilizia malekezo kwenye screen kisha roboot(washa) simu yako na utakuwa umefanikiwa ku-flash Revosoft Project X Rom na utapata muonekano wa S5 kwenye S4 yako.
Endapo wewe mtumiaji wa Samsung Galaxy S4 GT-I9500 na ungependa kuipa muonekano kama wa S5 basi wasiliana nasi kupitia namba +255753618318 au +255716203029 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000.
Mpaka hapo tumefikia mwisho, kama una swali lolote kuhusiana na hii mada basi toa maoni chini hapo na utajibiwa.
Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
Labels:
samsung
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment