Wengi wetu tumetumia computer zinazotumia window. Moja sifa kubwa za computer za window ni start menu. Najua wengi wetu wamekuwa wakijiuliza maswali kama inawezekana kuweka start menu kwenye simu zinazotumia android.
Taskbar ni application inayokuwezesha kuweka start menu kwenye simu za android. Tazama picha ya simu yangu ikiwa na start menu kama
JINSI YA KUWEKA START MENU YA WINDOW KWENYE SIMU ZA ANDROID
STEP 1
Hakisha simu yako ipo rooted. Ili kujua kama simu yako tayari imekuwa rooted au bado tembelea link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/11/jinsi-ya-kujua-kama-simu-yako-imekuwa.html
STEP 2
Hakikisha tayari umeweka Xposed Framework kwenye simu yako kama bado tembelea link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/07/maelekezo-jinsi-ya-kuweka-xposed.html
STEP 3
Download Taskbar application kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu yako
http://dl-xda.xposed.info/modules/com.rootuninstaller.taskbarw8_v2236_3d050c.apk
STEP 4
Baada ya kumaliza ku install Taskbar, kwenye simu yako fungua Xposed installer app na utapata muonekano kama huo hapo chini
STEP 5
Nenda kwenye kipengele cha modules kisha tick kibox pembeni ya Taskbar kama picha inavyoonyesha chini
STEP 6
Nenda kwenye kipengele cha framework kama kinavyo onekena kwenye step 4 juu kisha utapata muonekano kama huo hapo chini
STEP 7
Bonyeza sehemu iliyoandikwa install/update kisha reboot simu yako. Mpaka hapo utakufanikiwa kuweka Taskbar kwenye simu yako. Baada ya simu yako kuwaka tafuta kialama chenye muonekano kama nilichokizungushia duara la rangi nyekundu
Ukikibonyeza hicho kialama utapata muonekano kama huo hapo chini
Mpaka hapo tumefikia mwisho. Natumaini utakuwa umeelewa jinsi ya kuweka Taskbar kwenye simu yako.
No comments:
Post a Comment