Monday, August 22, 2016

JINSI YA KUPIMA KASI (SPEED) YA INTERNET KWENYE SIMU YAKO

Kujua speed ya internet kwenye simu yako ya android ni jambo la maana sana. Wengi wetu huwa tunapenda kuona speed kubwa ya internet lakin pale tunapotumia simu zetu hatuwezi jua speed au kasi ya internet.

Leo tutajifunza kaujanja kadogo ambacho katakuwezesha kujua speed ya internet kwenye simu yako. Zipo njia mbili ambazo unaweza kutumia kujua speed au kasi ya internet kwenye simu yako.

Njia ya kwanza ni kwakutumia Internet Speed Meter. Njia hii haitaji uwe ume root simu yako. Kwa wale ambao hawaja root simu zao wanaweza kutumia hii njia. Install hiyo app kisha fwata maelekezo.

Sasa twende kwenye ile njia ya pili ambayo ni ya wajanja. Njia hii inahitaji uwe ume root simu yako na pia uwe tayari umeweka Xposed Framework kwenye simu yako. Kama wewe hujaweka Xposed Framework kwenye simu yako basi tembelea link chini kujifunza jinsi ya kuweka Xposed Framework
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/07/jinsi-ya-kuweka-xposed-framework-kwenye.html

Kama wewe tayari una xposed framework kwenye simu yako, download kisha install Network Speed Indicator kwa kutumia link chini
http://dl-xda.xposed.info/modules/tw.fatminmin.xposed.networkspeedindicator_v16_a6bfd6.apk

Baada ya ku-install, nenda kwenye kipengele cha module kwenye Xposed Framework kisha weka tick kwenye kipengele cha Network Speed Indicator kama picha chini



Baada ya hapo restart (zima na kuwasha) simu yako. Ukiangalia juu utaona network speed indicator. Picha chini inaonyesha network speed indicator kwenye simu yangu na utaona speed ya internet yangu ikiwa 1.2 Mb/s wakati na download ikiwa na rangi ya njano. Hapo natumia wireless Internet(Wi-Fi) kutoka kwenye simu inayotumia vodacom 4G.

Kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment