Thursday, July 3, 2014
JINSI YA KUWEKA XPOSED FRAMEWORK KWENYE SIMU ZINAZO TUMIA ANDROID
Kama wewe unatumia simu yenye mfumo wa Android, nauwakika utapenda kujua kuhusiana na XPOSED FRAMEWORK. Kwa kifupi XPOSED FRAMEWORK ni njia inayokupa uwezo wa kubadilisha muonekano wa simu yako na kuipa simu yako uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Natumaini hapo utakuwa na maswali kibao jinsi gani unaweka XPOSED FRAMEWORK kwenye simu yako? Ni rahisi sana kuweka xposed framework kwenye simu yako.
Kabla ya kuelezea jinsi ya kuweka xposed framework kwenye simu yako tuangalie kwanza vigezo vinavyo itajika ili uweze kuweka xposed framework kwenye simu inayotumia android.
VIGEZO (REQUIREMENTS) VYA KUZINGATIA KABLA UJAWEKA EXPOSED FRAMEWORK
1)
Cha kwanza kabisa simu yako inatakiwa iwe inatumia android 4.0 (Ice Cream Sandwich) au zaidi ya hapo. Kama simu yako ipo chini ya android 4.0 basi hutaweza kuweka xposed framework kwenye simu yako.
2)
Simu yako inabidi iwe rooted. Rooted kwa kifupi ni njia inayompa uwezo mtumiaji wa simu ya android kufanya chochote kwenye simu yake. Kwa upande wa computer rooted ni kama kusema Administrator.Wote tunajua kwamba system admin ndiye mwenye uwezo wa kufanya chochote kwenye computer.
Simu kama HTC, Samsung au Sony huwa zinakuwa Unroot ili kumzuia mtumiaji asije akafanya maujanja yatakayopelekea kuaribu simu yake. Sasa kwakua sisi ni binadamu na tuna freedom inatubidi tuzi root simu zetu ili tuweze kuziongezea maujanja. I hope you got an idea about root and unroot. Kama ujaelewa basi google utaweza kupata more information
Sasa kama wewe unauwakika kwamba tayari simu yako ipo rooted na inatumia android 4.0 au zaidi basi endelea kusoma jinsi ya kuweka Exposed Framework kwenye simu yako.
MAELEKEZO JINSI YA KUWEKA EXPOSED FRAMEWORK
STEP 1
Download Xposed framework installer app Kisha install kwenye simu yako ya android. Ikimaliza ifungue kwenye simu yako. Simu yako itakuwa inaonekana kama hivi.
STEP 2
Bonyeza Framework Kisha install update. Ikimaliza Restart simu yako. Ukibonyeza Framework utaona picha kama hii
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka Exposed Framework kwenye simu yako. Ili kuipa simu yako maujanja sasa nenda kwenye kipengele cha Modules. Kipengele cha modules ndicho kinachokupa maujanja ili kuweza kubadilisha simu yako na kuipa uwezo mkubwa.Download Modules mbalimbali kisha zijaribishe kwenye simu ili kuona simu yako itakuwaje
Kama hujalewa tafadhali usifanye unaweza ukaaribu simu yako. Toa comment kama una swali. Piga +255716203029 au +255753618318 kama ungependa usaidiwe. Gharama zitatozwa (Tsh 25,000 tu.)
Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment