Thursday, August 18, 2016

APPS TANO ZA MUHIMU AMBAZO HUTAKIWI KUKOSA KAMA UME ROOT SIMU YAKO

Ku root simu ya Android ni jambo la muhimu sana maana utaweza kutumia simu yako jinsi unavyotaka. Moja ya faida kubwa unayoweza kupata endapo ume root simu yako ni uwezo wa kutoa System apps ambazo zinakujazia nafasi tu bure.

Mfano kwenye Samsung, kuna apps nyingi ambazo zinakuwa hazitumiki na ukitaka kuzitoa unakuwa unashindwa. Mfano ni Snote, Flipboard, SVoice, Samsung Geer, SHealth na nyingine nyingi. Endapo uta root simu yako basi utakuwa na uwezo wa kutoa apps kama hizo ambazo zinakuwa hazitoki kwenye simu yako.

Kwa wale ambao wanataka kujua faida au umuhimu wa ku root simu basi hakikisha unatembelea link chini
https://phonetricktz.blogspot.com/2015/11/faida-au-umuhimu-wa-ku-root-simu-za.html

Leo tutaongelea zile apps tano za muhimu ambazo hutakiwi kukosa kama ume root simu yako.

Titanium Backup

Titanium Backup ni moja yaa app muhimu sana ambayo hutakiwi kukosa kama ume root simu yako. Hii app itakusaidia kutoa apps ambazo haziwezi kutoka kwa njia ya kawaida, pia inakuwezesha kufanya apps ambazo zinatoka na kuwa hazitoki kwenye simu yako. Kwa kutumia hii apps utaweza ku backup apps zako kisha kuzi hifadhi na baadae kuja kuzirudisha. Pia hii app ni nzuri sana pale unapotaka kutoa virus kwenye simu yako. Unaweza download hii app kwa kutumia Link chini
http://nitroflare.com/view/AE7EDB46C694721/7wxwa.Titanium.Backup.Pro.7.4.0.1.Final.Full.rar

AdBlock Plus

Kama jina linavyosema, hii app ipo makini kuzuia matangazo kwenye simu yako. Watu wengi wanaotumia simu za android hukumbwa sana na hili tatizo la matangazo. Unakuta simu inakuonyesha matangazo bila ruksa yako wewe mtumiaji. Unaweza download hii app kwa kutumia link chini
https://adblockplus.org/en/android



Xposed Framework

Xposed Framework ni moja ya app ambayo ina mambo mengi sana na sitaweza kuyazungumzia mambo yote hapa. Kwa kifupi tu Xposed Framework inakusaidia kuboresha simu yako na kuifanya iwe na muonekano wa kipekee. Ni mambo mengi sana unaweza kufanya na hii app. Endapo unaitaji kujua Xposed Framework ni nini na unaiwekaje kwenye simu yako basi tembelea link chini
https://phonetricktz.blogspot.com/2014/07/jinsi-ya-kuweka-xposed-framework-kwenye.html

Unaweza download Exposed Framework kwa kutumia link chini
Kwa wenye android 5 na kuendelea tumia link chini
http://forum.xda-developers.com/showthread.php?t=3034811

Viper4Android

Viper4Android ipo kwa wale watu wanaopenda sauti kwenye simu zao. Kwa kutumia hii app utaweza ku set simu yako itoe sauti nzuri kwenye earphones zako na hata kwenye speaker za simu. Hii app inakuja na driver yake pamoja na equalizer na vionjo vingi ambazo vitakusaidia kupata good music kutoka kwenye simu yako ya android. Hii app inatumika kuanzia kwenye android 2.3 mpaka android 6. Unaweza download hii app kwa kutumia link chini
http://www.mediafire.com/download/ar5men9o5ar7inb/ViPER4Android_FX_v2401_A4.x-A6.x.apk

Flashify

Hii app ni kwa ajili ya wale wanaopenda ku flash simu zao kwa kutumia custom recovery. Hii app inakusaidia kupangilia mafile unayotaka kuflash na kuya flash moja moja bila kuzima simu yako. Hili ni jambo zuri sana kuhusu hii app. Pia inakusaidia kuflash vitu kama boot image bila hata kutumia adb commands. Hii app inauzwa lakin ukiitafuta kwenye google natumaini utapata ya magumashi.

Kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment