Saturday, November 21, 2015

FAIDA AU UMUHIMU WA KU ROOT SIMU ZA ANDROID

Najua wewe unaye soma hii babari utakuwa umeshawai kusikia neno ROOT kutoka kwa rafiki yako au pengine umekutana na hilo neno kwenye mitandao na pengine umekuwa ukijiuliza maswali kama kuna umuhimu au faida za kuroot simu ya android.

Kwa kifupi tu, leo tutaongelea faida au umuhimu wa kuroot simu za android na pia tutaeleza hasara unazoweza kuzipata baada ya kuroot simu yako ya android.

Kuroot simu maana yake ni kumuezesha au kumpa mamlaka yote mtuamiaji wa simu ya android kuongeza, kupunguza au kurekebisha mfumo mzima wa android software. Pengine hapo utakuwa unajiuliza mbona mimi naweza kutoa au kuongeza apps au kubadilisha settings za simu yangu bila hata kuroot simu?

Jibu ni kwamba uki root simu yako ya android utaweza kufanya mambo mengi sana kwenye simu yako na kuifanya simu yako iwe kama wewe unavyo taka. Mfano, unapo nunua simu yako dukani ikiwa mpya kabisa na baada ya kuiwasha utagundua tayari kuna apps zimekwa kwenye simu na unapo jaribu kuzitoa huwa hazitoki. Kwa mfano, simu za samsung huwa zina apps kama (chatOn, S voice, S Planner) na nyinginezo ambazo unakuta tayari zimeshawekwa kwenye simu na mdaa mwingine hauzitaji na ungependa uzitoe lakini hazitoki. Sasa hapo ndipo faida moja ya root inapokuja. Ukiwa ume root simu, basi utaweza kutoa app yoyote mdaa wowote bila kujali kama ilikuwepo pale uliponunua simu yako

Faida nyingine ya kuroot ni kuongeza ufanisi wa simu yako ya android. Mfano mzuri tazama picha chini. Picha ya kushoto ni My files (file manager) ambayo ipo kwenye simu aina zote za Samsung Galaxy S4. Picha ya kulia ni file manager ambayo natumia mimi kwenye samsung galaxy s4. Sasa utajiuliza mbona file manager yangu ni tofauti na ile iliyopo kwenye simu za samsung galaxy s4? Swali lingine linakuja kwamba file manager iliyopo upande wa kulia inatumika kwenye Samsung Galaxy S6 na S6 edge pamoja na Note 5. Sasa utajiuliza inawezekana vipi mimi kutumia file manager iliyopo kwenye S6 kwenye S4 yangu? Jibu ni kwamba uki root simu mambo kama hayo yanawezekana bila shida.



Faida nyingine ni kuipa ulinzi imara simu yako. Hapa nina maanisha hata kama simu yako imeingia baadhi ya apps ambazo zinahatarisha ulinzi wa simu yako basi kwa kupitia root utaweza kuziondoa mara moja. Kwa kweli faida za kuroot simu zipo nyingi sana. Una weza search google kuendelea kuzijua.

Sasa tuongelee kidogo baadhi ya hasara unaweza kuzipata baada ya kuroot simu yako ya android. Moja ya hasara kubwa ni kupoteza warranty. Kumbuka unaponunua simu dukani hupewa warranty kwamba endapo simu yako italeta shida basi utaweza rudisha na kutengenezewa bure au kupewa simu nyingine. Endapo uta root simu yako basi tayari utakuwa umepoteza warrant ya simu yako.

Hasara nyingine unayoweza kupata baada ya kuroot simu ni kuaribu simu yako. Zipo simu nyingi ambazo uki root vibaya hushindwa kuwaka na kusababisha hasara kubwa.

Kama umpenda kazi zeti usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment