Tuesday, November 24, 2015

APPS TANO BORA ZITAKAZO KUSAIDIA KUIHIFADHI PICHA, MUSIC, VIDEO NA DOCUMENTS ZAKO BURE

Zipo apps nyingi sana zinazo julikana kama online storage au cloud storage ambazo huwa zinakupa huwezo wa kuifadhi vitu vyako kama picha, video na documents zako bure.

Leo tutaziongelea hizi apps tano ambazo ni bora na zitakuwezesha kuifadhi files zote iwe ni music au video au picha hata documents bure na utaweza kuviona vitu vyako mdaa wowote bila kujali upo kwenye computer au tablet au smartphone

MEGA

Mega ni moja ya app inayojulikana sana kwa kuifadhi files zako zote iwe ni video, picha, music na documents bure. Endapo utajiandikisha (register) utapewa kiasi cha 50GB bure ili uifadhi files zako zote na utaweza kuziona mdaa wowote bila kujali unatumia tablet au computer au smartphone. Unaweza download Mega app kutoka kwenye play store kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=nz.mega.android



GOOGLE DRIVE

Wengi tunaijua Google Drive kwa maana kwa kuwa inapatika kwenye computer, smartphone na tablet. Siku za karibuni Google drive iliruhusu mtumiaji wa whatsapp kuweza ku backup chat kwenye google drive. Google Drive ni bure na unachotakiwa kuwa nacho ni email ya Gmail au kama una android phone basi sio tatizo. Google Drive inakupa hadi 15GB bure kuweka picha zako , video, music pamoja na documents na utaweza kuona vitu vyako muda wowote ule bila kujali upo kwenye computer au tablet au smartphone. Unaweza download Google Drive kupitia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.apps.docs



DROPBOX

Dropbox haina tofauti sana na Google Drive au Mega. Endapo utajiandikisha kwenye Dropbox basi utapata kiasi cha 2GB bure ili uweze kuifadhi files zako zote kama picha au video, music files, apps na utaweza kuvipangilia vitu vyako kwenye folders kama ilivyo kwenye computer. Dropbox inakuja na auto photo upload ambayo inakuifadhia picha zako palo utakapozipiga na camera yako. Unaweza download Dropbox kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.dropbox.android



MEDIAFIRE

Mediafire ni ya kitamboo sanaa na kwa wale wanaopenda ku download vitu huenda tayari wameshakutana na mediafire. Mediafire inakupa kiasi cha 10GB bure pale unapo jiandikisha. Utaweza kuzitumia hizo 10GB kuweka kitu chochote unachotaka iwe ni video au picha, music na files zingine bila kulipa chochote. Unaweza download mediafire kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.mediafire.android



MICROSOFT ONE DRIVE

Microsoft One Drive kwa jina lingine kama Skydrive ina kupa kiasi cha 5GB bure ili uweze kuweka documents zako kama word, powerpoint, spreadsheet, video, picha na vingine vingi. Skydrive ni muhimu sana kwa matumizi ya office. Unaweza download mediafire kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.microsoft.skydrive



Kwa wale wanaopenda kazi zetu mnaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment