Tuesday, August 30, 2016

JINSI YA KUTENGENEZA ANDROID APP (PART TWO)

Android ni mfumo (operating system) ambao ni maarafu sana kwa kuwa umefanikiwa kutumiwa kwenye vyombo vya kielectroniki kama simu, saa, tv, laptops, tablet na hata kwenye magari ya kisasa pia utakuta android.

Kwa wale ambao walikosa part one ya hili somo basi unaweza kutembelea link chini ili uweze kujua nini tulijifunza kwenye part one.
https://phonetricktz.blogspot.com/2016/08/jinsi-ya-kutengeneza-android-application.html

Leo tutajifunza jinsi ya kuakikisha computer yako ya window ipo tayari kabisa kuanza kutengeneza android app. Computer yako inatakiwa iwe na program mbili ambazo ni Java pamoja na Android Studio

JavaSe (Java Development Kit)

programming language ambayo inatumika kutengeneza Android app ni Oracle’s Java SE. Java SE ilitengenezwa na Sun Microsystems na baadae ikanunuliwa na Oracle. Zipo aina tatu za Java. Kuna Java EE (Java Enterprise Edition) ambayo hii hutumika kwenye network ya macomputer makubwa. Halafu kuna Java ME (Java Micro Edition) ambayo utumika kutengeneza mobile application. Java SE ina uwezo mkubwa kuliko Java ME na ndio inatumiwa na Google kutengeneza Android Os.

Ili kuweza kuweka JavaSe (Java Development Kit) kwenye computer yako unatakiwa kutembelea link chini kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Java download.
http://www.oracle.com/technetwork/java/javase/downloads/index.html



Baada ya kubonyeza download utapata muonekano kama picha chini kisha chagua unatumia aina gani ya window (64bit or 32bit) kisha kubali Accept License Agreement za oracle halafu utaanza ku download



Baada ya kumaliza ku-download, install Java Se kwenye computer yako.

Android Studio

Android Studio ndio program inayotumia kama IDE (integrated development environment). Inamaanisha kwamba shughuli nzima ya kutengeneza android app, kuijaribu na hata kuiweka kwenye playstore itafanyikia kwenye android studio. Android Studio imetengenezwa na Google ili kurahisisha shughuli za ku design android app. Unaweza download android studio kwa kutumia link chini kisha install kwenye computer yako
https://developer.android.com/studio/index.html



Kwa leo tutaishia hapa, muda mwingine tutajifunza jinsi ya kuanza kutumia Android Studio pamoja na jinsi ya kutengeneza android app.

Ukitaka kuendelea na hili somo bonyeza Part 3 chini

Kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment