Friday, November 21, 2014
JINSI YA KUBALISHA RANGI YA STATUSBAR PAMOJA NA VIALAMA KWENYE SIMU ZA ANDROID
Android inasifika kwa mambo mengi sana mojawapo ikiwa ni uwezo wa mtumiaji kubadilisha muonekano wa android na kuweka muonekano ambao yeye binafsi anaupenda
Leo tutajifunza jinsi ya rangi ya vialama vilivyo kwenye statusbar. Vialama hivyo ni kama alama ya battery, network, aina ya network pamoja na saa. Pia tutabadilisha rangi ya statusbar. Statusbar ni ile sehemu ya juu kabisa kwenye kioo chako cha simu. Sehemu iyo ndio inatumika kuonyesha notification za apps pamoja na kuonyesha alama ya network, battery etc.
Picha chini inaonyesha jinsi rangi ya statusbar pamoja na vialama vya battery, network, saa vilivyo badilika rangi
Kama umependa muonekano huo hapo juu na ungependa uweke kwenye simu yako soma maelekezo chini
JINSI YA KUBALISHA RANGI YA STATUS BAR PAMOJA NA VIALAMA VILIVYO KWENYE STATUSBAR
STEP 1
Hakikisha umeweka Gravity Box kwenye simu yako. Kama bado tembelea link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/11/jinsi-ya-kuweka-gravity-box-kwenye-simu.html
STEP 2
Fungua Gravity Box kwenye simu yako na utapata muonekano kama huo hapo chini
STEP 3
Bonyeza kipengele cha statusbar tweaks kisha utaona muonekano kama huo hapo chini
STEP 4
Bonyeza sehemu iliyoandikwa statusbar colors kisha enable icon colors utaona alama ya on kama picha hapo chini
SSTEP 5
Nenda kwenye kipengele cha statusbar background color na chagua rangi unayoipenda kama picha inavyoonyesha chini
STEP 6
Nenda kwenye kipengele cha statusbar icon color kisha fanya kama ulivyofanya kwenye step 5.
Mpaka hapo tumefikia mwisho natumaini utakuwa umeelewa. Kama umepata tatizo toa maoni yako chini na utajibiwa. Usiache ku like Facebook page yetu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment