Friday, November 21, 2014

JINSI YA KUWEKA GRAVITY BOX KWENYE SIMU ZA ANDROID.


Wengi tumekuwa tukitumia simu za android bila kujua kwamba unaweza kubadilisha muonekano mzima wa siku yako kwa kutumia application kama Gravity Box.

Gravity Box inakuwezesha kufanya chochote kwenye simu. Moja ya kitu kikubwa ambacho



Gravity Box inaweza kufanya ni kubadili rangi ya status bar pamoja na rangi ya network signals kama picha inavyoonyesha chini



Ukiangalia picha za juu kwa umakini utagundua kwamba rangi ya sehemu ambayo vialama vya network, battery vinapokaa imebadilika pamoja na rangi ya vialama hivyo. Rangi ya picha ya kwanza ni orange na nyeupe wakati picha ya pili ni nyeusi na njano iliyofifia.

Hiyo ni moja ya kazi ya gravity box. Sasa kama ungependa ujue jinsi ya kuweka gravity box kwenye simu  yako hakikisha unafwatilia  malekezo chini

JINSI YA KUWEKA GRAVITY BOX KWENYE SIMU ZA ANDROID

STEP 1
Hakisha simu yako ipo rooted. Ili kujua kama simu yako tayari imekuwa rooted au bado tembelea link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/11/jinsi-ya-kujua-kama-simu-yako-imekuwa.html

STEP 2
Hakikisha tayari umeweka Xposed Framework kwenye simu yako kama bado tembelea link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/07/maelekezo-jinsi-ya-kuweka-xposed.html

STEP 3
Download Gravity box kisha install kwenye simu yako.
Kwa wale wanaotumia android 4.4 na kuendelea download gravity box kupitia link chini
http://dl-xda.xposed.info/modules/com.ceco.kitkat.gravitybox_v119_86d3a3.apk

Kwa wale wanaotumia android 4.3 na chini ya hapo download gravity box kupitia link chini
http://dl-xda.xposed.info/modules/com.ceco.gm2.gravitybox_v113_facd71.apk

STEP 4
Baada ya kumaliza ku install gravity box, kwenye simu yako fungua Xposed installer app na utapata muonekano kama huo hapo chini


STEP 5
Nenda kwenye kipengele cha modules kisha tick kibox pembeni ya gravity box kama picha inavyoonyesha chini

STEP 6
Nenda kwenye kipengele cha framework kama kinavyo onekena kwenye step 4 juu kisha utapata muonekano kama huo hapo chini


STEP 7
Bonyeza sehemu iliyoandikwa install/update kisha reboot simu yako. Mpaka hapo utakufanikiwa kuweka gravity box kwenye simu yako. Nenda kafungue Gravity Box na utaona muonekano kama huo hapo chini


Tafadhali nakuomba usijaribu kuchezea kipengele kinachoitwa Navigation Bar Tweaks. Kama unataka kuchezea kipengele hicho hakikisha umefanya back up ya simu yako.

Ukitaka kubadilisha rangi ya statusbar pamoja na vialama vilivyomo kwenye statusbar nenda kwenye kipengele kinachosema StatusBar tweaks

Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi yangu usiache ku like Facebook  page.

No comments:

Post a Comment