Sunday, July 13, 2014

(NANI ZAIDI) KATI YA SAMSUNG GALAXY S5 NA HTC ONE (M8)



Samsung Galaxy S5 na HTC One M8 ni baadhi ya simu kali ambazo ni mpya kabisa na hazija maliza hata mwaka tangu zianze kuuzwa. Simu zote mbili zina RAM ya ukubwa wa 2GB zinatumia chip aina ya Qualcomm Snapdragon 801.

S5 ni Water, Dust resistant wakati HTC One M8 haijawa design kupambana na mazingira magumu kama kutumbukizwa kwenye maji. USB type ya S5 ni 3.0 wakati ya HTC One M8 ni 2.0. Hii ina maanisha S5 inaweza kuamisha vitu kwa kasi zaidi kupitia usb cable kushinda HTC One M8

 Display S5 ina ukubwa wa 5.1 inch wakati HTC One M8 ni 5 inch. Zote mbili ni 1080p resolution (FULL HD). Samoled ndiyo aina ya display iliyopo kwenye S5 na LCD3 ipo kwenye HTC One M8.

Kwa wale wanaopenda kuperuzi kwa speed basi simu zote mbili hizi zipo ready kwa ajili ya kazi kama hiyo. Zote ni 4G LTE.

Simu zote mbili zinatumia android 4.4.2. Pia zinauwezo wa kutumia Micro SDcard zenye ukubwa wa mpaka kufikia 128GB. Kwa maelezo mengine tafadhali angalia video chini.



Kama una swali toa maoni (comment) chini hapo na utajibiwa. Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+

No comments:

Post a Comment