Friday, September 9, 2016

JINSI YA KUTATUA TATIZO LA NO COMMAND KWENYE TECNO A7

Watumiaji wengi wa Tecno hukumbuna na matatizo kama simu zao kushindwa kuwaka pale wanapo update simu zao. Moja ya matatizo ambayo yanaweza kutokea pale unapo update simu yako ni simu kushindwa kuwaka na mda mwingine kuandika neno linalo sema No Command.

Leo tutajifunza jinsi ya kutatua tatizo la No command kwa simu za Tecno A7.

Vigezo na Masharti

  • 0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
  • 1: Hakikisha simu yako ni Tecno A7
  • 2: Computer inayotumia windows
  • 3: Hakikisha simu yako ina charge kuanzia 70%
  • 4: Hakikisha umeweka vcom driver kwenye computer yako
  • 5: Soma maelekezo yote kwa makini kisha ndio ujaribu kwenye simu yako

STEP 0

Hakikisha tayari umeweka vcom driver kwenye computer yako inayo tumia windows kama bado tembelea link chini kujia jinsi ya kuweka vcom driver kwenye computer yako
https://thebroodle.com/microsoft/windows/how-to-install-mtk65xx-preloader-usb-vcom-drivers-in-windows/

STEP 1

Download Tecno Firmware kwa kutumia link chini
https://docs.google.com/uc?id=0B260w8lc543AaVk0MGNldHlkSTg&export=download

STEP 2

Baada ya kumaliza ku download, lifungue (extract) hilo file ulilo download kwenye Step 1 na utapata mafile yanayo fanana kama kwenye picha chini

STEP 3

Download Sp Flash Tool na baada ya kumaliza ku download lifungue (extract) hilo file kwenye folder lolote kwenye computer yako. Ndani ya hilo folder double click file linaloitwa flashtool.exekama linavyo onekana kwenye picha chini

STEP 4

Nenda kwenye kipengele kinachosema Download kisha utapata muonekano kama picha chini. Kama hujapata muonekano kama picha chini rudia maelekezo tena

STEP 5

Bonyeza kipengele kinachosema Scatter-loading kama inavyo onekana kwenye picha chini

STEP 6

Computer itakwambia utafute file linaloitwa Android-Scatter. Kwa kutumia window mpya iliyofunguka kwenye computer yako, Nenda kwenye lile folder ambalo uli extract file ulilo download kwenye Step 2 kisha chagua file linaloitwa MT6735_Android_scatter.txt kisha bonyeza Open kama inavyo onekana kwenye picha chini

STEP 7

Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama kwenye picha chini. Kama ujapata muonekano kama kwenye picha chini, tafadhali rudia tena maelekezo.

STEP 8

Bonyeza kipengele kinachoitwa Download kama kwenye picha chini

STEP 9

Zima simu yako, kisha chomeka USB kwenye computer yako halafu chomeka kwenye simu yako. Kisha subiri mpaka utakapopata ujumbe unao sema OK kama kwenye picha chini

Kama ujapata muonekano kama picha juu basi hakikisha umefwatilizia maelekezo vizuri. Kama ukishindwa unaweza wasiliana nasi kupitia whatsapp number +255627732383.. Pia unaweza kutufwata kwenye instagram yetu kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment