Monday, July 28, 2014

(MAELEKEZO) ROOT SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100


Root ni kitu muhimu sana kwenye simu zinazo tumia mfumo wa android. Bila ku root simu yako hautaweza kufurahia simu yako. Kitu kizuri kuhusu android ni uwezo wa kuibadilisha na kuongeza vitu vizuri kwenye simu yako.

Sasa leo ntatoa maelekezo mafupi ambayo yatakuwezesha ku root SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100. Endapo utafanikiwa ku root simu yako basi utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutumia custom rom na hata Exposed Framework.

Kabla sijatoa maelekezo ni vyema nikupe masharti ambayo unatakiwa kukubaliana nayo kabla uja root simu yako


(VIGEZO NA MASHARTI)

1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.

2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer

3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100

4: You need common sense and brain.

5: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window

6) utakuwa umepoteza warranty ya simu yako endapo uta root simu yako.

JINSI YA KU ROOT SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100

STEP 0 
 Hakikisha model ya simu yako ni SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100. Kama ni tofauti basi usi root unaweza haribu simu yako.


STEP 1
Download file hapo chini kisha liweke kwenye memory card ya simu yako
DOWNLOAD LINK | File name: SU-BB-Installer.zip (1.14 MB)

STEP 2
Washa simu yako kwenye recovery mode. Kama hujui jinsi ya kuwasha simu yako kwenye recovery mode basi soma maelekezo chini
 unatakiwa kuizima simu yako kisha Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) mpaka utakapoana
Galaxy S2 logo ndio uwachie.

STEP 3
Chagua kipengele kinachosema Install Update from External Storage

 Note: Tumia cha kuongeza sauti au kupunguza kwenda kwenye menu unayoitaka, kisha tumia cha kuwashia kuchagua menu.


STEP 4
Chagua lile file uliloweka kwenye memory card (SU-BB-Installer.zip) baada ya hapo utaona section inayokwambia uchague kati ya yes au no. wewe chagua yes.

STEP 5
Reboot simu yako baada ya kumalizika.

STEP 6
Done. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa ku root SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100.

Endapo kama wewe ungependa usaidiwe basi wasiliana nasi kupitia namba +255753618318 au +255716203029 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000.
 
Kama una swali toa maoni (comment) chini hapo na utajibiwa. Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+ 

1 comment:

  1. Je namna ya kuongeza android version ya simu nafanyaje???

    ReplyDelete