Watu wengi wanaotumia simu za android bado hawajaweza kuzitumia simu zao kwa asilimia mia moja. Kwa wale wanaotumia SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100 leo nitawaonyesha njia ya kuweza kutumia simu zao zaidi kushinda wanavyotumia kwa sasa.
Leo nitatoa maelekezo jinsi ya kuweka custom recovery kwenye SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100. Kuna aina nyingi za custom recovery lakini mimi nitaiongelea PHILZ TOUCH RECOVERY.
Faida moja kubwa ya kuweka custom recovery kwenye simu yako ni kuweza ku-flash ROM tofauti tofauti na kuongeza ufanisi kwenye simu yako. Zipo faida nyingi sana. Ukitaka kujua faida nyingine basi wewe check google.
Bila kuongea sana, tupate maelekezo jinsi ya kuweka custom recovery kwenye SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100
NOTE: (VIGEZO NA MASHARTI)
1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100.
4: U need common sense na brain.
5: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window
6: Install Samsung kies kwenye compuer yako ili kupata drivers za samsung galaxy s2. Samsung Kies inapatikana HAPA. Hakikisha unadownload kies na sio kies3
MAELEKEZO YA KUWEKA PHILZ TOUCH RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100
STEP 0
Hakikisha kama simu yako ni model GT-I9100. Kama ni tofauti na hiyo tafadhali usiendelee unaweza ukaharibu simu yako.
STEP 1
Download Odin program DOWNLOAD
STEP 2
Download Philz Touch Tar file DOWNLOAD
Kisha liweke hilo file kwenye desktop.
STEP 3
Extract/Unzip Odin zip file, Latest Odin3 v3.09.zip kwenye computer yako kwa kutumia (7-zip free software, au Win Rar) ili upate hili file. Odin3 v3.09.exe kisha liweke kwenye desktop pamoja na lile file ambalo umelidownload kwenye step 2
STEP 4
Double-click the Odin3 v3.09.exe file to open Odin
STEP 5
Izime simu yako kisha subiri kama sekunde 10.Washa simu yako ya samsung galaxy s2 kwenye download mode.
Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode bonyeza kitufe cha katikati (Home) + cha kupunguza sauti (Volume down) + na cha kuwashia (power) kisha vishikilie kwa pamoja mpaka utakapoana kwenye screen yako maneno yanayosema Press Volume Up now to continue to Download Mode. Sasa achia halafu bonyeza cha kuongeza sauti. (Volume up)
Hakikisha simu yako inamuonako kama picha inavyoonyesha chini kabla ujaendele kwenye step 6.
STEP 6
Kwenye computer yako hakikisha uko kwenye ile Odin program ambayo uli double click kwenye step 4. Sasa chomeka simu kwenye computer ikiwa bado kwenye download mode kwakutumia usb cable na Odin itaitambua simu yako na itaonyesha message kama inavyoonekana kwenye picha
STEP 7
Kwenye Odin Click AP button na chagua lile file ambalo uli download kwenye step 2 ambalo uliliweka kwenye desktop. Jina la file ni : philz_touch_6.43.4-i9100.tar.md5. Muekano wako kwenye computer utakuwa hivi endapo utakuwa umenifwatilia vizuri. Tafadhali naomba Odin yako kwenye computer iwe na muonekano kama huo. Viboksi ambavyo vinatakiwa viwe na alama ya vema ni Auto Reboot na F.Reset Time kama inavyoonekana kwenye picha.
STEP 8
Kabla ya kuendelea hakikisha tupo pamoja. Usiendele kama ujaelewa.
STEP 9
Kwenye Odin bonyeza start button ambayo ipo chini kabisa kisha subiri mpaka utakapoana Odin imekuandikia PASS kama picha inavyoonyesha chini. Chomoa simu yako kwenye computer kisha subiri mpaka itakapowaka yenyewe kama ikichelewa kuwaka basi bonyeza cha kuwashia na itawaka kama kawaida.
STEP 10
Hongera mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako ya galaxy s2 na utakuwa na uwezo wa kuflash rom mbalimbali ili kupata muonekano mzuri na kuongeza ufanisi zaidi. Ili kuhakikisha simu yako ina custom recovery basi zima simu yako kisha subiri kama sekunde kumi. Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano. Endapo utafanikiwa basi simu yako itakuwa hivi
Tumia cha kuongeza sauti na kupunguza sauti kufika kwenye menu unayoitaji kisha bonyeza cha kuwashia (power) kuchagua menu.
Endapo kama wewe ungependa uweke custom recovery kwenye simu yako na hauwezi basi wasiliana nasi kupitia namba +255753618318 au +255716203029 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000.
Kama una swali toa maoni (comment) chini hapo na utajibiwa. Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
No comments:
Post a Comment