Thursday, June 26, 2014

(VIDEO) ANDROID SIO KWENYE SMARTPHONES TU SASA HADI KWENYE MAGARI (ANDROID AUTO), SAA (ANDROID WEAR) NA TV(ANDROID TV)


Ni masaa 24 tu yamepita tangu Google kuonyesha mipango yao ya technology kwa upande wa smartphones, saa na magari. Kama ulikosa Google O/I iliyofanyika jana basi tutaweza kukupa vidokezo vya vitu ambavyo vilivyo ongelewa.

Google wameanzisha android auto ambayo itatumika kwenye magari. Dhumuni kubwa la kuweka android kwenye magari ni kurahisisha maisha ya binadamu hasa kwenye upande wa mawasialiano.




Google pia ilitangaza android one ambayo itawawezesha makampuni kama HTC, LG, MOTOROLA, SAMSUNG kutengeneza simu za bei rahisi ambazo zitauzwa chini ya $100 sawa na Tsh 165000. Kwa kufanya hivi Google itaweza kufikia malengo yake ya kupata watuamiaji wa android billion 5 tofauti na sasa ambao ni 1 billion.

Kwa upande wa saa, Google wameanzisha android wear ambayo itatumia kwenye smart watch. LG, Motorola na Samsung ndio makampuni ya kwanza kutoa saa ambazo zinatumia mfumo wa android wear.

Angalia video chini kujua mengi kuhusiana na android auto, android wear, android L na android tv

No comments:

Post a Comment