Kwa wale wenye Samsung galaxy note 2 GT- N7100 sasa wanaweza kuzigeuza simu zao na kupata muonekano wa kisasa wa Samsung Galaxy Note 3. Hii inamaanisha utakuwa unatumia apps za samsung ambazo zipo kwenye galaxy note 3 na Samsung Galaxy S5.
Baadhi ya apps ambazo utazipata kwenye Note 2 ni
- S5 Toolbox feature
- S5 Power Saving Mode
- S5 Ultra Power Saving Mode
- S5 Lockscreen Effects
- S5 System UI
- S5 Launcher with Magazine & Pullup app
- S5 Wallpaper
- Note 3 Icons
- Note 3 MyFiles
- Note 3 SNote
- Note 3 ScrapBook
- Note 3 SketchBook
Hizi nazo ni baadhi ya picha zikionyesha Samsung Galaxy Note 2 GT N7100 ikiwa na muonekano wa Galaxy Note 3.
Bila kuongea maneno mengi tuzungumzie kwanza vitu vya kuzingatia kabla ujajaribu hu ujanja kwenye Samsung Galaxy Note 2 yako
REQUIREMENTS ( VIGEZO VYA KUZINGATIA)
1: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy Note 2 GT-N7100 na sio vinginevyo.
2: Hakikisha una custom recovery kama Philz touch recovery kwenye Samsung Galaxy Note 2 GT-N7100. Kama wewe hujui ni maana ya Custom Recovery na ungependa kuiweka kwenye Note 2 GT-N7100 yako basi tembelea hii link BONYEZA HAPA.
3: Hakikisha Galaxy note 2 yako inatumia android 4.3 au zaidi na sio chini ya hapo
3: Unaelewa English japokuwa nitajitahidi kupunguza kutumia lugha ya kingereza kadri niwezavyo.
4: Hakikisha simu yako ina charge ya kutosha. Mapendekezo yangu simu yako iwe na charge kwanzia 70% na kuendelea
5: Hakikisha Memory Card yako ina nafasi isiyopungua 2GB.
6: You need common sense and brain
NOTE : MIMI SITAUSIKA ENDAPO UTAHARIBU SIMU YAKO. CONTINUE ON YOUR OWN RISK
MAELEKEZO YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY NOTE 2 GT N7100 IWE KAMA NOTE 3
STEP 0
Hakikisha kama simu yako ni model GT N7100. Kama ni tofauti na hiyo tafadhali usiendelee unaweza ukaharibu simu yako.
STEP 1
Download DN3(Ditto Note 3) ROM HAPA kisha baada ya kumaliza kudownload liweke hilo file kwenye memory card ya simu yako. Naomba hilo file usilifungue, liweke kama lilivyo.
Jina la file ni DN3_v5.2_by_E-Team.zip Ukubwa wa file ni 1.84GB.
STEP 2
Zima simu yako kisha subiri kama sekunde 10. Washa simu yako kwenye Recovery Mode. Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye recovery mode unatkiwa ufanye hivi (Simu yako ikiwa tayari umeizima Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano na utaona recovery)
Note: tumia kitufe cha kuongeza sauti na cha kupunguza sauti kupanda na kushuka kwenye menu na bonyeza kitufe cha kuwashia kuchagua menu
STEP 3
Ukiwa bado kwenye Recovery fanya backup(nandroid backup) ya simu yako kwa kwenda kwenye kipengele cha backup and restore kisha backup. Hakikisha pia unafanya backup ya efs folder.
Note: backup itachukua muda kidogo hakikisha unasubiri mpaka simu yako itakapomaliza kubackup. Backup itakusaidia kurudisha simu yako kama ilivyokuwa mwanzoni endapo utataka kurudisha simu yako kwenye hali yake ya mwanzoni.
STEP 4
Baada ya kumaliza Ku-backup na simu yako ikiwa bado kwenye recovery mode nenda kipengele cha Wipe data/Factory reset kisha chagua YES.
Note: Kufanya Wipe data/Factory reset ni muhimu sana kuhakikisha simu yako haipati matatizo kama bootloop
STEP 4
Baada ya kumaliza ku-wipe/factory reset, nenda kwenye kipingele cha install zip kwenye recovery kisha chagua install zip from SD CARD halafu nenda kachague lile file ambalo ulidownload kwenye step 1 ambalo uliliweka kwenye memory card yako. Hakikisha jina la file ni DN3_v5.2_by_E-Team.zip
STEP 5
Fwatilizia malekezo kwenye screen kisha roboot(washa) simu yako na utakuwa umefanikiwa ku-flash DN3_v5.2_by_E-Team.zip na utapata muonekano wa S5 na Note 3 kwenye Note 2 yako
Kama umeshindwa kuelewa malekezo niliyoyatoa basi tazama video ikikuonyesha jinsi ya KUIFANYA SAMSUNG GALAXY NOTE 2 GT N7100 IWE KAMA NOTE 3
Endapo wewe mtumiaji wa Samsung Galaxy Note GT-N7100 na ungependa kuipa muonekano kama wa note 3 basi wasiliana nasi kupitia namba +255753618318 au +255716203029 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000.
Mpaka hapo tumefikia mwisho, kama una swali lolote kuhusiana na hii mada basi toa maoni chini hapo na utajibiwa.
Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
No comments:
Post a Comment