Kwa wale wenye simu za android wanaweza kuzipendezesha simu zao zikiwa zina mvuto mzuri kwa kuweka floating window. Kwa wale wanaotumia simu za samsung kama S4, S5 na Note3 floating window au mult-tasking ni kitu cha kawaida.
Haya maelezo ni kwa wale ambao hawana simu za Samsung lakini wanapenda kuwa na floating window au mult-tasking kwenye simu zao. Mimi natumia HTC sensation na nimefanikiwa kuweka floating window kwenye simu yangu na nimefurahishwa kuona floating window kwenye simu yangu.
Picha zikionyesha Muonekano wa simu yangu ambayo nimefanikiwa kuweka floating window na halo
VIGEZO VYA KUZINGATIA KABLA UJAWEKA FLOATING WINDOW NA HALO KWENYE SIMU YAKO
1) Hakikisha simu unayotaka kuweka floating window siyo Samsung.
2) Hakikisha umeweka exposed framework kwenye simu yako. Kama ujaweka exposed framework basi tembelea HAPA kujua jinsi ya kuweka exposed framework kwenye simu yako.
3) Hakikisha Simu yako ipo rooted. Kama hujui maana ya rooted, tembelea HAPA kupata intro
4) Mimi sitahusika endapo utaharibu simu yako. Continue on your own risk. Nakushauri ufanye backup (nandroid) kabla ujajaribu. Ili kufanya nandroid backup unabidi uwe na custom recovery.
Kama simu yako ina vigezo vyote nilivyovitaja hapo juu basi unaweza endelea.
(MAELEKEZO) JINSI KUWEKA FLOATING WINDOW NA HALO KWENYE SIMU YA ANDROID
STEP 1
Download halo apk kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.paranoid.halo
STEP 2
Download Xhalo floating window.apk kwa kutumia link chini.
http://dl-xda.xposed.info/modules/com.zst.xposed.halo.floatingwindow_v240_d6490b.apk
STEP 3
Sasa ukiwa kwenye simu yako install Halo.apk file ambalo ulidownload na kuliweka kwenye memory card kwenye step 1.
STEP 4
Fungua exposed framework kwenye simu yako kisha nenda modules na chagua Xhalo Floating Window kama picha inavyoonyesha chini. Hakikisha una reboot simu yako.
Fungua Halo app kwenye simu yako kisha pin application ambazo ungependa ziwe zinaelea kwenye home screen yako. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka HALO NA XHALO FLOATING WINDOW KWENYE SIMU YAKO.
Kama ujaelewa basi tazama video chini ambayo inatoa malekezo jinsi ya kuweka halo na floating window kwenye simu yako.
Kama hujalewa tafadhali usifanye unaweza ukaaribu simu yako. Toa comment kama una swali. Piga +255716203029 au +255753618318 kama ungependa usaidiwe. Gharama zitatozwa (Tsh 25,000 tu.) Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
No comments:
Post a Comment