Sunday, June 29, 2014

(MAELEKEZO) WEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S3 I9300, I9305


Custom Recovery ni njia kuu inayo kuwezesha wewe mtumiaji wa Samsung Galaxy S3 I9300 au I9305 kuweza ku-flash rom tofauti tofauti kwenye simu yako. Kwa kifupi hautaweza kutumia Custom Rom kama hauna Custom Recovery kwenye simu yako

Leo nitatoa maelekezo jinsi ya kuweka custom recovery (PHILZ TOUCH RECOVERY) kwenye Samsung Galaxy S3 I9300. Hakikisha unasoma malekezo yote halafu ndio ujaribu kwenye simu yako.




NOTE: (VIGEZO NA MASHARTI)

1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S3 GT-I9300.
4: You need common sense and brain.
5: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window
6: Install Samsung kies kwenye compuer yako ili kupata drivers za samsung galaxy S3. Samsung Kies inapatikana HAPA. Hakikisha unadownload kies na sio kies3

MAELEKEZO YA KUWEKA PHILZ TOUCH RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S3 GT-I9300

STEP 0
 Hakikisha kama simu yako ni model GT-I9300. Kama ni tofauti na hiyo tafadhali usiendelee unaweza ukaharibu simu yako. 

 STEP 1
 Download Odin program zip file   DOWNLOAD   

STEP 2
 Download Philz Touch Tar file   DOWNLOAD
 Likimaliza kujidownload likopi na uliweke kwenye desktop ya computer yako
Jina la file utakalodownload ni philz_touch_6.41.6-i9300.tar.md5

 STEP 3
Unakumbuka lile file ulilo-download kwenye step1 (Odin zip file, Latest Odin3 v3.09.zip)? sasa lifungue (Extract/Unzip) kwenye computer yako kwa kutumia (7-zip free software,  au Win Rar) ili upate hili file. Odin3 v3.09.exe kisha liweke kwenye desktop pamoja na lile file ambalo umelidownload kwenye step 2
 
STEP 4 
Double-click the Odin3 v3.09.exe file to open Odin

STEP 5 
Izime simu yako kisha subiri kama sekunde 10.Washa simu yako ya samsung galaxy s3 kwenye download mode. Tazama picha chini kisha soma maelekezo chini ya picha kujua jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode


Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode bonyeza kitufe cha katikati (Home) + cha kupunguza sauti (Volume down) + na cha kuwashia (power) kisha vishikilie kwa pamoja mpaka utakapoana kwenye screen yako maneno yanayosema Press Volume Up now to continue to Download Mode. Sasa achia halafu bonyeza cha kuongeza sauti. (Volume up)

Hakikisha simu yako inamuonako kama picha ya kulia inavyoonyesha chini kabla ujaendele  kwenye step 6.


STEP 6 
 Kwenye computer yako hakikisha uko kwenye ile Odin program ambayo uli double click kwenye step 4.  Sasa chomeka simu kwenye computer ikiwa bado kwenye download mode kwakutumia usb cable na Odin itaitambua simu yako na itaonyesha message kama inavyoonekana kwenye picha chini



STEP 7
Kwenye Odin Click  AP button na chagua lile file ambalo uli download kwenye step 2 ambalo uliliweka kwenye desktop. Jina la file ni : philz_touch_6.41.6-i9300.tar.md5.  

Muekano wako kwenye computer utakuwa hivi endapo utakuwa umenifwatilia vizuri. Tafadhali naomba Odin yako kwenye computer iwe na muonekano kama huo. Viboksi ambavyo vinatakiwa viwe na alama ya vema ni Auto Reboot na F.Reset Time kama inavyoonekana kwenye picha.



STEP 8 
Kabla ya kuendelea hakikisha tupo pamoja. Usiendele kama ujaelewa. 

STEP 9
Kwenye Odin bonyeza start button ambayo ipo chini kabisa kisha subiri mpaka utakapoana Odin imekuandikia PASS kama picha inavyoonyesha chini. Chomoa simu yako kwenye computer kisha subiri mpaka itakapowaka yenyewe kama ikichelewa kuwaka basi bonyeza cha kuwashia na itawaka kama kawaida.



 STEP 10
 Hongera mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako ya galaxy s3 na utakuwa na uwezo wa kuflash rom mbalimbali ili kupata muonekano mzuri na kuongeza ufanisi zaidi. 

Ili kuhakikisha simu yako ina custom recovery basi zima simu yako kisha subiri kama sekunde kumi. Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano. Endapo utafanikiwa basi simu yako itakuwa na muonekano ambao unafana na picha inavyoonyesha chini.



Endapo kama wewe ungependa uweke custom recovery kwenye simu yako na hauwezi basi wasiliana nasi kupitia namba +255753618318 au +255716203029 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000.

Kama una swali toa maoni (comment) chini hapo na utajibiwa. Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+

No comments:

Post a Comment