Thursday, May 29, 2014

JINSI YA KUONDOA TATIZO LA " NOT ENOUGH SPACE" KWENYE SAMSUNG GALAXY SII I9100


Kama wewe unatumia samsung galaxy s2 i9100 na umekuwa ukipata tatizo la "not enough storage" ukiwa unajaribu kuweka apps mpya kwenye simu yako basi tatizo ni rahisi kutatulika.
.
Kwa kifupi Samsung Galaxy S2 ina ukubwa wa 16GB lakini katika hizo 16GB kuna 14GB ambazo zipo free. Ndani ya hizo 14GB zimegawanyika mara mbili. Kuna Device memory na USB storage.

Sasa ukiwa unaweka apps mpya huwa zinatumia hiyo nafasi ya Device Storage ambayo huwa na 2GB. Endapo utaweza kujaza hiyo 2GB basi utakuwa uwezi tena kuweka apps na utakuwa unapata hii error "not enough storage" kila ukiwa unajaribu kuweka au ku-update apps

Sasa haya ni maelekezo yakufanya ili kuweza kuondoa hilo tatizo la "not enough storage". Kwakifupi hapa tunachofanya ni kuongeza ukubwa wa device storage(2GB) hadi kufikia (6GB) na USB Storage itabakiwa na 8GB.

NOTE : MIMI SITAHUSIKA ENDAPO UTAHARIBU SIMU YAKO

Vitu unavyotakiwa uwenavyo

1: Computer inayotumia window.
2: USB cable ya samsung galaxy s2
3: hakikisha una install Kies kwenye computer yako. Unaweza kuipata hapa download
4: Hakikisha una utaalamu kidogo wa computer
5: Haya maelezo ni kwa ajili ya SAMSUNG GALAXY SII I9100

Sasa soma kwanza maelekezo yafuatayo mpaka mwisho, ukiona umeelewa basi unaweza kuendelea kwa kufanya kwa vitendo. Kila hatua nitaweka picha ili uweze kuelewa unachokifanya kwa usahihi

STEP 1
Download ODIN 1..85 program hapa download
STEP 2
Download Philz CWM Recovery ya Galaxy S2 kutoka hapa
STEP 3
Download mafaili ya Partition kutoka hapa
STEP 4
Tafadhali hamisha mafile yako yote yaliyopo kwenye simu kama picha, video, etc na yaifadhi kwenye memory card au kwenye computer yako kwasababu kila kitu kwenye simu yako kitafutika
STEP 5
Sasa fungua lile file ambalo umeli-download kwenye step 1 kwa kutumia winrar au 7zip na kisha double click program ya Odin3 v1.85 na itafunguka kama inavyoonekana kwenye picha


STEP 6
Sasa extract lile file ambalo umedownload kwenye step 3 na kisha liweke kwenye desktop na muonekano wake wa ndani wa hilo folder itakuwa hivi


STEP 7
Lile file ambalo ulidownload kwenye step 2, hakikisha na lenyewe unaliweka kwenye desktop kama lilivyo. Naomba hili file usilifungue wa usili-edit. Liweke kama lilivyo

STEP 8
Zima simu yako. Kisha iweke simu yako kwenye download mode kwa kubonyeza na kuvishikilia kitufe cha kupunguza sauti(volume down) + Home(kitufe cha katikati) + Power ( kitufe cha kuwashia) vyote kwa pamoja kwa sekunde kama nne au tano halafu achia. Kama simu yako itakuonyesha Press volume up key basi bonyeza tu cha kuongeza sauti. Ukifanikiwa kwenye hii step basi simu yako itaonyesha hivi kwenye screen

STEP 9
Sasa fungua ile program ya Odin3 v1.85 ambayo ulikwisha ifungua kwenye step 5 kisha Chomeka simu yako kwenye computer kwa kutumia usb cable yake na kisha subiria hadi Odin itambue simu yako. Ikitambua simu yako basi utaona kwa pembeni mkono wa kushuto kiboksi kimoja kimekuwa cha njano kama inavyoonekana kwenye picha.

STEP 10
Kwenye Odin yako tazama button iliyoandikwa PDA kisha click utaona window nyingine imefunguka halafu nenda desktop chagua lile file ambalo ulilodownload kwenye step 2 na kuliweka kwenye desktop (step 7). Endapo utafanikiwa basi kwenye Odin yako itaonekana hivi


STEP 11
Pale pale tena kwenye Odin bonyeza button iliyoandikwa PIT kisha chagua file linaloitwa 6GB pit ambalo lipo ndani ya folder linaloitwa (4gb_6gb_8gb_Pit_Files) ambalo pia uliliweka kwenye desktop pale ulipokuwa Step 6. Kama ujaelewa tafadhali rudia tena step 6. Kumbuka hapa tumechagua 6GB pit file ili kuongeza ukubwa wa device memory kutoka kwenye 2GB hadi 6GB. Kama utataka iwe 8GB basi chagua file la 8GB pit. Endapo utafanikiwa kumaliza hii step basi kwenye computer yako itakuwa hivi





STEP 12
Kabla ujaendelea basi hakikisha odin yako kwenye computer ipo kama hii inayoonekana kwenye picha. Kama haipo hivyo basi hakikisha tena kwa umakini kabla ujaendelea.



 STEP 13
Bonyeza button ya start kwenye odin kisha subiri mpaka uone imekuandika PASS. Chomoa simu yako kwenye computer halafu iwashe. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuondoa tatizo la "not enough storage". Kwenye simu yako nenda kwenye settings kisha nenda kwenye storage halafu angalia ukubwa wa device memory na ule wa usb storage.

Endapo kama utashindwa na utataka msaada basi piga namba +255716203029 na utasaidiwa kurekebishiwa kwa kiasi cha Tsh 25,000 tu.Kama unaswali lolote basi toa comment yako chini na utajibiwa.

Please usisahai ku like facebook na google+ ili kuendelea kupata habari njema kuhusu simu za android.

No comments:

Post a Comment