Samsung Galaxy S3 ni moja ya simu kali sana na bado bei yake ni kubwa licha ya kuwa ni toleo la kizamani. Endapo kama ungependa uendelee kuifurahia samsung galaxy s3 huna budi kuifanyia rooting ili uweze kutumia vitu kama exposed framework au hata kuweka custom rom.
Sasa leo ntatoa maelekezo mafupi ambayo yatakuwezesha ku root SAMSUNG GALAXY S3 GT-I9300 . Endapo utafanikiwa ku root simu yako basi utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutumia custom rom na hata Exposed Framework.
Kabla sijatoa maelekezo ni vyema nikupe masharti ambayo unatakiwa kukubaliana nayo kabla uja root simu yako
(VIGEZO NA MASHARTI)
1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S3 GT-I9300
4: You need common sense and brain.
5: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window
6) utakuwa umepoteza warranty ya simu yako endapo uta root simu yako.
JINSI YA KU ROOT SAMSUNG GALAXY S2 GT-I9100
STEP 0
Hakikisha model ya simu yako ni SAMSUNG GALAXY S3 GT-I9300. Kama ni tofauti basi usi root unaweza haribu simu yako.
STEP 1
Download CF-AUTO-ROOT kisha extract hilo file ili kupata mafile haya
- CF-Auto-Root-m0-m0xx-gti9300.tar.md5
- Odin3-v1.85.exe
Double click on Odin3-v1.85.exe kufungua Odin program
STEP 3
Sasa zima simu yako kisha iwashe kwenye downloading mode. Kama ujui jinsi ya kuwasha kwenye downloading mode tazama picha chini kisha soma maelekezo
Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode bonyeza kitufe cha katikati (Home) + cha kupunguza sauti (Volume down) + na cha kuwashia (power) kisha vishikilie kwa pamoja mpaka utakapoana kwenye screen yako maneno yanayosema Press Volume Up now to continue to Download Mode. Sasa achia halafu bonyeza cha kuongeza sauti. (Volume up)
Hakikisha simu yako inamuonako kama picha ya kulia inavyoonyesha chini kabla ujaendele kwenye step 4.
STEP 4
Connect Galaxy S3 kwenye computer yako kwakutumia usb cable.
Note:
Endapo simu yako itakuwa connected vizuri basi utaona message inayosema "ADDED" kwenye program ya odin. Odin yako kwenye computer itaonekana hivi
STEP 5
Kwenye Odin program bonyeza button iliyoandikwa PDA kisha chagua file linaloitwa CF-Auto-Root-m0-m0xx-gti9300.tar.md5 ambalo ulilipata kwenye step 2. Kama hujui hili file lilipo basi rudia tena step 2. Hakikisha program yako ya odin ina muonekano kama picha hapo chini. Hakikisha kibox kimoja tu kinachoitwa auto root ndio kina alama ya vyema kama picha inavyo onyesha chini.
STEP 6
Kama umeridhika na kazi yako na unauwakika tupo sambamba basi click button ya START kwenye Odin kisha subiri mpaka utakapopata message inayosema PASS kama picha inavyoonekana chini
STEP 7
Simu yako itazima na kujiwasha kisha chomoa usb cable. Baada ya simu yako kuwaka utagundua SuperSU app imekuwa installed kwenye simu yako.
Endapo kama wewe ungependa usaidiwe ku-root simu yako, basi wasiliana nasi kupitia namba +255753618318 au +255716203029 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000.
Kama una swali toa maoni (comment) chini hapo na utajibiwa. Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
No comments:
Post a Comment