Tuesday, August 9, 2016

JINSI YA KUTUMIA ADB (ANDROID DEBUG BRIDGE) KWENYE SIMU ZA ANDROID

Android Debug Bridge (adb) sio neno geni kwa wale wapenzi wa simu za android. Android Debug Bridge (adb) ni mfumo ambao unakuwezesha kuweza kuongea na simu ya android kwa kutumia computer. Adb ni client server program ikimanisha kwamba huwa inafanya kazi kwenye upande wa chombo cha mtumiaji wa mwisho kama laptop.

Leo tutajifunza jinsi ya kuweka adb kwenye computer yako ili uweze kufanya computer yako iweze kuongea na simu yako kwa kutumia command prompt program iliyopo kwenye computer yako.

Adb ina faida nyingi sana na kama wewe ni mtumiaji wa simu za android unapaswa kujua jinsi ya kutumia adb. Moja ya faida kubwa ya adb ni kuirekebisha simu yako ya android pale inapoleta matatizo. Mfano kwenye simu za Tecno, kama C8 ukienda kwenye recovery utaona kipengele kinachoitwa apply update from adb kama picha inavyo onekana chini. Kutoka na mfano tunaweza kuona faida nyingine ya adb ni kuweza ku-push update kwenye simu yako ya android. Faida nyingine ni kwamba utaweza kuweka na kutoa program kutoka kwenye simu yako.

STEP 1

Download Minimal adb kwa kutumia link chini
https://www.androidfilehost.com/?fid=24521665358595410

STEP 2

Baada ya kumaliza ku-download Minimal adb, install kwenye computer yako kisha ifungue hiyo program na utapata muonekano kama picha chini

STEP 3

Chukua simu yako ya android kisha nenda kwenye Settings halafu tafuta developer options kama inavyo onekana kwenye picha chini

STEP 4

Bonyeza kipengele cha developer options kisha hakikisha Developer options ipo on na USB debugging ipo on kama kwenye picha chini

STEP 5

Chomeka simu yako kwenye computer kwa kutumia Usb. Kisha nenda kwenye ile program uliyo ifungua pale kwenye Step 2. Kisha andika hili neno

adb devices




kwa kuandikia adb devices ni kuhakikisha kwamba computer yako ina mawasiliano na simu uliyochomeka maana kama ukisoma picha juu utaona baada ya kuandika adb devices computer imekujibu na kukwambia list of device attached na utaona namba ya device yako.

adb reboot


Hii command inapeleka ujumbe kwenye simu yako na kufanya simu yako ijizime na kujiwasha.

adb


Hii command itakujulisha command zote zinazohusiana na adb na zinafanya kazi gani kwenye simu yako..

fastboot reboot-bootloader


Hii command inapeleka ujumbe kwenye simu yako na kufanya simu yako ijizime na kujiwasha kwenye bootloader. Kwa zile simu zenye Bootloader kama HTC basi utaweza kutumia hiyo command.

fastboot


Hiyo command itakupa msaada kujua command zinazo husiana na fastboot na jinsi ya kuziandika kwa usahihi

Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment