Tuesday, August 9, 2016

JINSI YA KUWEKA NEXUS LAUNCHER KWENYE SIMU YAKO YA ANDROID

Nexus ni simu ambazo zinatengezwa na kusambazwa na Google. Simu hizi huwa zinapewa kipao mbele sana na Google hasa pale android mpya inapotoka. Simu za nexus hupata updates kutoka google kwa haraka zaidi ukilinganisha na simu nyingine

Ndani ya simu za Nexus huwa zina launcher kama ilivyo kwenye simu nyingine. Siku chache Launcher mpya ambayo google wanatarajia kuiweka kwenye simu mpya ya nexus imevuja kwenye mitandao. Kizuri zaidi hiyo launcher unaweza kuijaribu kwenye simu yako ya android.

JINSI YA KUWEKA NEXUS LAUNCHER KWENYE SIMU YAKO YA ANDROID

STEP 0

Download Nexus launcher kwa kupitia link chini
https://www.androidfilehost.com/?fid=24588232905722237

STEP 1

Baada ya kumaliza ku-download liweke hilo file kwenye memory card yako kisha washa simu yako kwenye custom recovery kisha install zip halafu chagua hilo file uliloweka kwenye memory card.

STEP 2

Kwa wale ambao hawana custom recovery, unachotakiwa kufanya ni kulifungua hilo file ulilo download kisha install hiyo app kawaida. Endapo utatumia hii njia basi launcher yako itakosa alama ya G iliyopo juu kushoto kama inavyo onekana kwenye picha chini



Uzuri ulipo katika hii launcher ni kwamba ina uwezo wa kugeuka kufwatana na display yako ulivyo iweka. Kama inavyo onekana kwenye picha chini



Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment