Thursday, August 11, 2016

JINSI YA KUIFUFUA TECNO C8 AMBAYO HAIWAKI

Inauma sana pale unapoona simu yako ya Tecno C8 inawaka lakin inaishia kwenye neno Tecno halafu inakwamia hapo. Watu wengi sana wanapata matatizo kama haya lakin hawajui cha kufanya.

Leo tutajifunza jinsi ya kurekebisha simu ya Tecno C8 ambayo inawaka lakin inaishia kwenye neno Tecno. Njia tutakayo tumia leo inaitwa adb sideload. Kabla ujafanya chochote hakikisha tayari ume install Minimal adb kwenye computer yako. Kama bado ujaweka Minimal adb kwenye computer yako basi tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka minimal adb kwenye computer ya windows
https://phonetricktz.blogspot.com/2016/08/jinsi-ya-kutumia-adb-android-debug.html

Vigezo na Masharti

  • 0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
  • 1: Hakikisha simu yako ni Tecno Camon C8
  • 2: Computer inayotumia windows
  • 3: Hakikisha simu yako ina charge kuanzia 70%
  • 4: Hakikisha umeweka vcom driver kwenye computer yako
  • 5: Soma maelekezo yote kwa makini kisha ndio ujaribu kwenye simu yako

STEP 0

Hakikisha tayari umeweka vcom driver kwenye computer yako inayo tumia windows kama bado tembelea link chini kujia jinsi ya kuweka vcom driver kwenye computer yako
https://thebroodle.com/microsoft/windows/how-to-install-mtk65xx-preloader-usb-vcom-drivers-in-windows/

STEP 1

Download Tecno Firmware kwa kutumia link chini
https://mega.nz/#!UNwWTahA!y-z394qeOOxnoxrWgefBTe9vLqPjL_fTib6pGUMDMNw

STEP 2

Baada ya kumaliza ku-download, liweke hilo file ulilo download kwenye program folder la Minimal adb ambayo ume install mapema. Folder la minimal adb linakuwa na path C:\Program Files (x86)\Minimal ADB and Fastboot. Kwa hiyo ndani ya folder la Minimal adb litakuwa na muonekano kama picha chini

br/>
NOTE
Hakikisha una muonekano kama picha juu. File ambalo limekuwa highlighted na rangi ya blue ndio ambalo umedownload kwenye STEP 1. Kama folder lako la Minimal adb halina muonekano kama picha juu basi tafadhali rudia kusoma maelekezo tena


STEP 3

Washa simu yako ya Tecno C8 kwenye recovery mode. Ili kuwasha simu yako kwenye recovery mode unatakiwa ushikilie cha kuwashia na cha kuongeza sauti kwa pamoja na usiviachie mpaka simu yako itakapo onyesha logo ya Tecno kwenye display ndipo uviachie kama picha inavyo onekana chini

STEP 4

Subiri mpaka utakapo ona simu yako inafanana kama picha chini,

STEP 5

kisha bonyeza na kushikilia cha kuwashia kama sekunde mbili halafu bonyeza cha kuongezea sauti huku ukiwa umeshikila cha kuwashia na utapata muonekano kama picha chini. Kama ujapata muonekano kama picha chini rudia tena

STEP 6

Bonyeza cha kupunguza sauti mpaka utakofika kipengele kinachosema apply update from adb kisha bonyeza cha kuwashia. Kisha chomeka simu yako kwenye computer kwa kutumia usb cable. Kwenye computer yako fungua program Minimal adb ambayo uli install mapema. Baada ya kufungua minimal adb utapata muonekano kama picha chini



STEP 7

Andika hilo neno chini kwenye computer yako Kisha bonyeza Enter

adb devices


utapata muonekano kama picha chini.



STEP 8

Baada ya hapo andika hilo neno chini kisha bonyeza Enter

adb sideload Tcard_update_20160425.zip


kwenye simu yako baada ya mdaa utaona muonekano kama picha chini



Endapo utapata muonekano kama picha juu basi utakuwa umefanikiwa kuifufua simu yako ambayo ilikuwa inawaka inaishia kwenye neno Tecno. Simu yako itachukua muda kuwaka kwahiyo ipo muda kama dakika 15.

Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment