Friday, November 14, 2014

WHATSAPP MPYA INAKUWEZESHA KUFANYA MTU ASIJUE KAMA UMESOMA MESSAGE ZAKE


Week iliyopita whatsaap iliboreshwa(updated) na kumfanya mtu ajue kwamba tayari message alizokutumia umezipata na kuzisoma kwa kuonyesha vitiki viwili vya rangi ya blue kama picha inavyoonyesha chini.






Hali hiyo imesababisha utata mwingi kwenye jamii huku watu wengine wakipa divorce wengine kuachana na boyfriend au girlfriend kwasababu eti kaona message zake halafu kauchuna... hahaa.

Kutoka na hali hiyo whatsapp imeboreshwa (updated) na sasa inakuwezesha kuzuia hivyo vitiki vya blue na kufanya mtu asijue kama tayari umeshaaoma message zake.

Whatsapp hii mpya bado haipo kwenye playstore lakini kama wewe unatumia simu za android unaweza kuidownload kutoka kwenye website ya whatsapp au unaweza bonyeza link chini ku download sasa
http://www.whatsapp.com/android/current/WhatsApp.apk

Baada ya ku download whatsapp  na kuiweka kwenye simu yako ifingue kisha nenda kwenye settings na utapata muonekano kama huo hapo chini



Baada ya hapo nenda kwenye kipengele cha account kisha utapata muonekano kama huu hapa chini

Baada ya hapo nenda kwenye kipengele cha privacy na utapata muonekano kama huo hapo chini



Kwenye kipengele cha Read receipts utaona pamewekewa alama ya tick ikiashiria kwamba mtu atajua kama tayari umesoma message zake kwa kuonyesha vitiki viwili vya rangi ya blue.

Kama wewe utakuwa hutaki mtu ajue kama umesoma message zake alizokutumia unaweza ukakitoa hicho tick kwa kukibonyeza. Mpaka utakuwa umefanikiwa kumzia mtu asijue kama umesoma message zake.

No comments:

Post a Comment