Wednesday, May 27, 2015

JINSI YA KUTUMIA ACCOUNT MBILI ZA INSTAGRAM KWENYE SIMU MOJA


Instagram ilianzishwa mwaka 2010 na Kevin Systrom pamoja na Mike Krieger. Mwaka wa 2012 tayari instagram ilikuwa ishapata watumiaji wengi duniani kote. Mwaka huo huo kampuni ya Facebook ili nunua mtandao wa kijamii wa instagram kwa kiasi cha dollar za kimarekani $1billion.

Instagram ni moja wa mtandao wa kijamii unao kuwa kwa kasi ukilinganisha na mitandao mingine kama Google+. Licha ya kukua kwa kasi,Instagram imejikuta ikiingiza pesa nyingi kila mwaka ukilinganisha na mitandao mingine.

Tukirudi kwenye instagram, wengi huwa tunapata shida sana pale unapokuwa na account mbili za instagram halafu una simu moja. Huwa inakulazimu ku logout kwanza kisha ndio uweze ku login.

JINSI YA KUTUMIA ACCOUNT MBILI ZA INSTAGRAM KWENYE SIMU MOJA

STEP 1
Sasa kama unataka kutumia instagram mbili kwenye simu moja unachotakiwa kufanya ni kudownload Instwogram app kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu yako.

STEP 2
Ifungue instwogram app kisha login kwa kutumia account yako nyingine.

Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kutumia account mbili za instagram kwenye simu moja.

Kwa wale wanaopenda blog yetu na wanataka tuendele zaidi basi usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz


No comments:

Post a Comment