Wednesday, January 6, 2016

JINSI YA KUWEKA ANDROID 4.4.4 KWENYE SAMSUNG GALAXY S4 SGH-I337

Samsung Galaxy S4 SGH-I337 imekuwa ikisumbua watu sana pale wanapotaka ku update ili iweze kutumia android 4.4.4 au 5.0.1. Moja sababu inayopelekea simu hii kuwa tatizo pale unapotaka ku update ni kufungwa (locked) na makampuni ya simu kama AT&T pamoja na T-mobile.

Leo tutaona jinsi ya ku update Samsung Galaxy S4 SGH-I337 kutoka android 4.2.2 hadi kufikia android 4.4.4 na baadae nitatoa maelekezo jinsi ya kuweka android 5.0 kwenye Samsung Galaxy S4 SGH-I337.

JINSI YA KUWEKA ANDROID 4.4.4 KWENYE SAMSUNG GALAXY S4 SGH-I337

Vigezo na Masharti

  • 1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.

  • 2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer

  • 3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S4 (SGH-I377)

  • 4: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window

  • 5: Unatakiwa uwe na memory card yenye nafasi zaidi ya 1GB

  • 6: Hakikisha umeweka samsung driver kwenye computer

  • 7: Hakikisha simu yako ina charge zaidi ya 80%


STEP 0

Download (4.4.2)-Stock NB1--I337UCUFNB1 firmware kwa kutumia link chini. Tengeneza folder kwenye computer yako kisha liweke hilo file ndani ya folder ulilo tengeneza
https://www.mediafire.com/?ad73k3c1wj31cuo

STEP 1

Download ODIN V3.10.6 program kwa kutumia link chini kisha liweke hilo file ndani ya folder ulilo tengeneza kwenye Step 0.
http://www.mediafire.com/download/s46jpd0gl8v1jom/Odin.zip

STEP 2

Extract ODIN V3.10.6 program humo humo ndani ya folder

STEP 3

Kwenye simu yako nenda kwenye settings kisha tafuta kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyo onekana chini. Kama hicho kipengele haukioni basi nenda kwenye about phone kisha shuka chini mpaka utakapoona kipengele kinachosema build number kisha kibonyeze haraka haraka kama mara saba kisha rudi tena kwenye setting na uangalie kama developer options imetokea

STEP 4

Fungua developer options kisha hakikisha umeiwasha (turn on) halafu umeweka tick ua umekiwasha kipengele kinachosema USB debugging kama picha inavyo onekana chini.

STEP 5

Zima simu yako kisha iwashe kwenye Download Mode. Kama hujui jinsi ya kuwasha simu yako kwenye Download Mode unachotakiwa kufanya ni zima (turn off) simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuwashia (power button) na cha kupunguza sauti(vol down button)} mpaka simu itakapowaka kama picha inavyo onekana chini ndipo uachie vitufe vyote kwa pamoja.

STEP 6

Bonyeza kitufe cha kuongeza sauti kwenda kwenye Download Mode na utapata muonekano kama picha chini. Endapo una wasiwasi kwamba simu yako itaaribika au unaogopa na unataka simu yako irudi kama kawaida basi bonyeza kitufe cha kupunguza sauti au toa battery kisha rudishia kisha washa simu yako. Kama wewe hugopi na unataka kuendelea basi endelea kufwatilizia maelekezo

STEP 7

Rudi ndani ya lile folder ulilotengeneza kwenye Step 0, kisha double click ile program inayoitwa odin ambayo ulipata baada ya ku extract. Endapo upo sahihi utapata muonekano kama picha chini kwenye computer yako

STEP 8

Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy S4(SGH-I337) halafu chomeka kwenye computer kisha kwenye program ya odin utaona kibox kinarangi kimeandikwa com(xx) na neno linalosema added kama picha chini

STEP 9

Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file linaloitwa I337UCUFNB1_I337-4.4.2(Farsat Sagvan).tar ambalo uli download kwenye Step 0 kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.



Note
Hakikisha program yako ya odin ina fanana na picha juu kwa zaidi ya asilimia 98%. Haikisha vitiki kwenye program yako ya odin vina fanana na vyangu

STEP 10

Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.

STEP 11

Simu yako itazima na kujiwasha. Chomoa USB yako kutoka kwenye computer. Subiri zaidi ya dakika 7 kwa maana simu yako itachelewa kuwaka. Baada ya simu yako kuwaka nenda kwenye about phone kisha tazama kama android yako imebadilika kutoka 4.2.2 hadi kufikia 4.4.2

STEP 12

Download (4.4.4) NJ4 OTA Update -- 2400258.zip kwa kutumia link chini kisha weka hilo file kwenye memory card ya simu yako. Hakikisha hilo file hauliweki ndani ya folder lolote.
http://www.mediafire.com/download/aeir6x31djr7f3v/4.4.4%28Farsat_Sagvan%29.zip

STEP 13

Zima simu yako kisha iwashe kwenye recovery mode. Kama ujui jinsi ya kuwasha simu yako kwenye recovery mode unachotakiwa kufanya ni kuzima simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuongeza sauti(vol up button)} na cha kuwashia (power button) mpaka simu itakopo onyesha logo ya Samsung kisha viachie vitufe kwa pamoja. Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama picha chini.

STEP 14

Kwa kutumia kitufe cha kupunguza sauti nenda hadi kwenye kipengele kinachosema apply update from external storage kisha bonyeza cha kuwashia. Endapo utakuwa sahihi utakuwa na muonekano kama picha chini

STEP 15

Kwa kutumia kitufe cha kupunguza sauti nenda hadi kwenye kipengele kinachosema 4.4.4(Farsat Sagvan).zp kisha bonyeza kitufe cha kuwashia na usubiri mpaka simu yako itakapomaliza halafu itazima na kujiwasha yenyewe. Kuwa mvumilivu subiri mpaka simu yako itakopowaka kisha nenda kwenye about phone tazama kama android yako kama imefika 4.4.4. Simu ikiwa ina install itakuwa na muonekano kama picha chini

Mpaka hapo tumefikia mwisho, kama unataka kusaidiwa ku update Samsung Galaxy S4 SGH-I337 au simu yoyote unaweza kutucheck kwenye kupitia namba +255753877552 au +255753877552

Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ambayo ni phonetricktz au unaweza like facebook yetu.

STEP 17

No comments:

Post a Comment