Thursday, January 7, 2016

JINSI YA KUZUIA PICHA UNAZOTUMIWA KWENYE WHATSAPP ZISIONEKANE KWENYE GALLERY

Wengi wetu tumekuwa tukituma picha na kupokea picha kwa kutumia Whatsapp na picha zote unazotumiwa huwa zinaonekana kwenye gallery ya simu yako. Je ulishawai jiuliza kama kuna njia ya kuzuia picha unazotumiwa kwenye Whatsapp zisitokee kwenye Gallery?

Siku ya leo tutajifunza njia ya kufanya ili kuzuia picha unazotumiwa kwa Whatsapp zisitokee kwenye Gallery. Hii ni njia nzuri ya kuwazuia watoto au marafiki wasione picha unazotumiwa kwenye whatsapp pale wanapofungua gallery ya simu yako

JINSI YA KUZUIA PICHA UNAZOTUMIWA KWENYE WHATSAPP ZISIONEKANE KWENYE GALLERY

STEP 0

Download Es File Explorer kutoka kwenye play store

STEP 1

Fungua Es File Explorer kisha nenda kwenye device storage halafu tafuta folder linaloitwa Whatsapp kama picha inavyo onekana chini

STEP 2

Fungua folder la Whatsapp kisha ndani utoka folder linaloitwa media. Fungua folder la media kisha utapata muonekano kama picha chini

STEP 3

Ndani ya folder la media utaona folder linaitwa Whatsapp Images. Fungua folder la Whatsapp Images kisha juu kabisa kulia bonyeza vidoti vitatu na utapata muonekano kama picha chini

STEP 4

Bonyeza kipengele kinachosema New kisha bonyeza kipengele kinachosema file na kisha andika hili neno .nomedia kama picha inavyo onekana chini halafu bonyeza ok.
Nenda kwenye gallery kisha tazama kama utaona folder la Whatsapp au picha yeyote uliyotumia kwenye Whatsapp. Kama bado zipo basi zima na kuwashasimu yako. Endapo utataka picha zako za Whatsapp zionekane kwenye gallery basi nenda kafute lile file linaloitwa .nomedia ambalo ulilitengeneza kwenye Step 4.

Mpaka hapo tumefikia mwisho wa maelekezo. Kama unataka kuwasiliana nasi kuhusiana na tatizo lolote kwenye simu yako ya andorid basi wasiliana nasi kwa kutumia namba +255753877552. Pia unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment