Friday, January 8, 2016

TUMIA WHATSAPP KIJANJA NA CHAT HELPER

Whatsapp ni moja ya mtandao wa kijamii ambao una watumiaji zaidi ya 1 billion. Kwenye play store Whatsapp imekuwa downloaded zaidi ya 1 billion. Whatsapp imekuwa moja ya njia inayotumiwa na watu wengi kuwasiliana pamoja na kutumiana picha na video.

Chat Helper ni app ambayo itakusaidia kuweza kutumia whatsapp kirahisi sana. Chat Helper ina hesabu Whatsapp zote ambazo zimetumwa lakini bado huja zisoma na hutengeneza widget ndogo pembeni ikikuonyesha idadi za Whatsapp ambazo bado ujazisoma.

Ili kuelewa zaidi tazama picha chini na utaona ki box kulia ambayo kina alama ya Whatsapp na namba 7. Namba saba inatoa tarifa kwangu kwamba nimetumiwa Whatsapp 7 na bado sijazisoma. Uki bonyeza hicho ki box kitakupeleka moja kwa moja kwenye whatsapp.

JINSI YA KUWEKA CHAT HELPER

STEP 0

Download Chat helper kwenye play store au tumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=here.in.spark.chathelper

STEP 1

Baada ya kumaliza ku install fungua chat helper halafu hakikisha kipengele kinachosema Accessibility Service kipo on kama picha chini

STEP 2

Simu yako itakupeleka kwenye Accessibility upande wa settings halafu kibonyeze kipengele cha chat helper ambacho kitakuwa chini kabisa kisha hakikisha ume kiwasha ( turn on )

STEP 3

Endapo utapata ujumbe unaosema create widget basi hakikisha una tick kibox kinachosema always allow.

STEP 4

Kwenye kipengele cha visibility kina maanisha kwamba app zote ambazo zimewekewa alama ya vyema( tick ) ndizo ambazo kibox cha chat helper kitakuwa kinaonekana. Kwa mfano mimi sipendi hicho ki box kiwe kinaoneka nikiwa kwenye play store basi ntahakikisha natoa alama ya vyema kwenye kipengele cha play store kama picha chini

Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka chat helper kwenye simu yako na itakurahisishia pale unapotaka kutumia whatsapp.

Kama unapenda kazi zetu unaweza ukatufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment