Monday, January 11, 2016

JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY NOTE 2 (SHV-E250S)

Samsung Galaxy Note 2 (SHV-E250S) ni smartphone yenye uwezo mkubwa sana na ufanisi wake wa kazi ni mkubwa na wakuridhisha. Simu hii ina uwezo wa 32GB kama ukubwa wa kuhifadhi mafile yako pia ina 2GB ya RAM.

Ili uweze kuhifurahia vizuri Samsung Galaxy Note 2 (SHV-E250S) itakubidi uweke custom rom ili kuweza kubadili muonekano na kuongeza ufanisi zaidi. Ili kuweza kuweka custom rom itakubidi kwanza uwe tayari umeweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy Note 2 (SHV-E250S). Leo tutaona jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy Note 2 (SHV-E250S)

Note
Ili kujua recovery ambayo imekuja na simu yako unachotakiwa kufanya ni kuzima simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuwashia (power button) na cha kuongeza sauti(vol up button)} mpaka simu itakopo onyesha logo ya Samsung kisha viachie vitufe kwa pamoja. Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama picha chini.

Lengo kubwa ambalo tunataka tulifanye ni kutoa recovery ambayo imekuja na simu yako kama inavyo onekana juu kwenye picha na kuweka custom recovery ambayo itakusaidia kufanya mambo mengi kama kuweka custom rom, backup & restore & ku flash mods mbalimbali na mambo mengine mengi

JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY NOTE 2 (SHV-E250S)


Vigezo na Masharti

  • 1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.

  • 2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer

  • 3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY NOTE 2 (SHV-E250S)

  • 4: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window


STEP 0

Download Samsung usb drivers kwa kutumia link chini kisha install kwenye computer yako
http://www.devfiles.co/download/AbRa7wHc/SAMSUNG_USB_Driver_for_Mobile_Phones.exe

STEP 1

Download ODIN program kwa kutumia link chini kisha tengeneza folder kwenye desktop yako. Liweke hilo file ulilo download ndani ya folder
http://dl.sammobile.com/Odin3_v3.10.7.zip

STEP 2

Download TWRP recovery kwa kutumia link chini na mara baada ya kumaliza ku-download liweke hilo file ndani ya folder ulilotengeza kwenye Step 1.
http://www.techerrata.com/file/twrp2/t0ltetmo/openrecovery-twrp-2.7.2.0-t0ltetmo.img.tar

STEP 3

Rudi kwenye lile folder ulilotengeneza kwenye Step 1, Extract ile program (odin3_v3.10.7) uliyo donwload kwenye Step 1 humo humo ndani ya folder.

STEP 4

Kwenye simu yako nenda kwenye settings kisha tafuta kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyo onekana chini. Kama hicho kipengele haukioni basi nenda kwenye about phone kisha shuka chini mpaka utakapoona kipengele kinachosema build number kisha kibonyeze haraka haraka kama mara saba kisha rudi tena kwenye setting na uangalie kama developer options imetokea

STEP 5

Fungua developer options kisha hakikisha umeiwasha (turn on) halafu umeweka tick ua umekiwasha kipengele kinachosema USB debugging kama picha inavyo onekana chini.

STEP 6

Zima simu yako kisha iwashe kwenye Download Mode. Kama hujui jinsi ya kuwasha simu yako kwenye Download Mode unachotakiwa kufanya ni zima (turn off) simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuwashia (power button) na cha kupunguza sauti(vol down button)} mpaka simu itakapowaka kama picha inavyo onekana chini ndipo uachie vitufe vyote kwa pamoja.

STEP 7

Bonyeza kitufe cha kuongeza sauti kwenda kwenye Download Mode na utapata muonekano kama picha chini. Endapo una wasiwasi kwamba simu yako itaaribika au unaogopa na unataka simu yako irudi kama kawaida basi bonyeza kitufe cha kupunguza sauti au toa battery kisha rudishia kisha washa simu yako. Kama wewe hugopi na unataka kuendelea basi endelea kufwatilizia maelekezo

STEP 8

Rudi ndani ya lile folder ulilotengeneza kwenye Step 1, kisha double click ile program inayoitwa odin ambayo ulipata baada ya ku extract. Endapo upo sahihi utapata muonekano kama picha chini kwenye computer yako

STEP 9

Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy NOTE 2 (SHV-E250S) halafu chomeka kwenye computer kisha kwenye program ya odin utaona kibox kinarangi kimeandikwa com(xx) na neno linalosema added kama picha chini

STEP 10

Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file linaloitwa openrecovery-twrp-2.7.2.0-t0ltetmo.img.tar ambalo uli download kwenye Step 2 kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.



Note
Hakikisha program yako ya odin ina fanana na picha juu kwa zaidi ya asilimia 98%. Haikisha vitiki kwenye program yako ya odin vina fanana na vyangu

STEP 11

Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.

STEP 12

Chomoa USB yako kwenye computer. Ili kuona recovery mpya iliyopo kwenye simu yako basi rudia kama ulivyofanya pale ulipokuwa unataka kuangalia recovery ambayo imekuja na simu yako. Recovery mpya itakuwa na muonekano kama picha chini

Mpaka hapo tumefikia mwisho, kama unataka kusaidiwa kuwekewa custom recovery kwenye Galaxy Note 2 (SHV-E250S) au simu yoyote unaweza kutucheck kwenye Viber au Tango kupitia namba +255753877552

Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ambayo ni phonetricktz au unaweza like facebook yetu.

No comments:

Post a Comment