Monday, January 11, 2016

JINSI YA KUZUIA BAADHI YA PICHA NA VIDEO ZISIONEKANE KWENYE GALLERY

Siku chache zilizopita tuliona ujanja ambao utakuwezesha kufanya picha unazotumiwa kwenye whatsapp zisitokee kwenye Gallery. Leo tutaona jinsi ya kuzuia folder lolote lenye picha na video lisiweze kuonekana kwenye gallery.

Hii ni njia nzuri sana kuwakomesha wale watu wanaopenda kuangia kwenye gallery na kuanza kuangalia picha zako bila ridhaa yako. Muda mwingine hata wazazi hupenda kushika simu na kuanza kuangalia picha kwenye gallery na muda mwingine unakuta una video na picha zenye utata na hupendi mzazi wako azione. Sasa njia ipo ya kuzuia hayo mambo kama hayo yasikupate

JINSI YA KUZUIA BAADHI YA PICHA NA VIDEO ZISIONEKANE KWENYE GALLERY

STEP 0

Download Es Explorer kutoka kwenye play store au tumia link chini kuweza ku download
http://www.apkmirror.com/wp-content/themes/APKMirror/download.php?id=53753

STEP 1

Fungua Es file Explorer app kisha tengeneza folder halafu nenda kaamishe picha zako zote pamoja na video ambazo hupendi mtu yeyote azione pale anapofungua gallery yako

STEP 2

Baada ya kuamisha picha na video zote, fungua tena hilo folder ulilotengeza kwa kutumia Es File Explorer kisha bonyeza vidoti vitatu juu kulia kama picha chini inavyo onekana

STEP 3

Bonyeza kipengele kinachosema New kisha bonyeza kipengele kinachosema file na kisha andika hili neno .nomedia kama picha inavyo onekana chini halafu bonyeza ok.


Nenda kwenye gallery yako na utagundua picha na zile video ulizoamisha hazipo na hazionekani kwenye gallery

Kama unapenda kazi zetu unaweza ukatufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment