Friday, March 31, 2017

KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA KUHUSU SAMSUNG DEX

Samsung Dex ni kifaa ambacho kimezinduliwa na samsung siku chache zilizopita wakati Samsung Galaxy S8 na S8+ zikiwa zinazinduliwa.

Hichi kifaa kitakuwezesha mtumiaji wa Samsung Galaxy S8 na S8+ kuweza kuamisha screen ya simu yako na kwenda kwenye monitor au hata Tv yenye HDMI support. Hichi kifaa kinakuja na HDMI port, USB-TYPE C port, Ethernet jack .

Ili kuweza kuelewa zaidi tazama video chini ikionyesha jinsi Samsung Dex itakavyokuwa inafanya kazi.



Picha chini inaonyesha muonekano wa Samsung Dex Samsung sio wa kwanza kufanya kitu kama hichi pia microsoft tayari walishajaribu kuanzisha kufanya mambo kama haya. Samsung wanadai wanashirikia na microsoft kuona jinsi watakavyo iboresha samsung dex kuwa  applications nyingi na kuwa kama desktop computer. Hichi kifaa kitaanza kuazwa tarehe 21 April kwa kiasi cha $149 (Tsh 335,000)

Mpaka hapa tumefikia mwisho. Usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya #phonetricktzili kuwa kwanza kupata habari mbali mbali kuhusiana na teknologia. Pia usiache kutembelea website mpya ya phonetricktz ili uweze kujifunza vitu kiundani zaidi.

No comments:

Post a Comment