Thursday, June 12, 2014

(MAELEKEZO) JINSI YA KUINGIA KWENYE RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S3 NA SIMU NYINGINE ZA SAMSUNG


Wale ambao hawajui nini maana ya recovery mode basi leo nitatoa maelezo kidogo kuhusiana na recovery mode.

Simu nyingi zinazotumia mfumo wa android huwa zinakuwa na recovery mode. Kama jina livyosema "Recovery" hii ni sehemu muhimu sana kwenye simu yako na inakupa uwezo wa kurekebisha simu yako endapo itakuwa inakupa matatizo madogo madogo.

Kwa mfano, Samsung Galaxy S3 inakuja na recovery na jinsi ya kuingia kwenye recovery kwenye Samsung galaxy s3 ni rahisi sanaa. Kuingia kwenye recovery mode haiwezi kuleta madhara yoyote kwenye simu yako bali utakuwa umeijua simu yako kiundani zaidi.

JINSI YA KUINGIA KWENYE RECOVERY KWA WALE WANATUMIA SAMSUNG GALAXY S3 NA SIMU NYINGINE ZA SAMSUNG



1) Zima simu yako (Power off your device).

2)Shikilia cha kuongeza sauti (vol up) + Home (cha katikati) + Cha kuwashia (power) kwa muda wa   kama wa sekunde tano kisha achia cha kuwashia huku ukiwa umeendelea kushikilia cha kuongeza sauti (vol up) + Home (cha katikati). Baada ya muda mfupi utaona screen yako inaoneka kama hapo kwenye picha chini.


Tumia cha kuongeza na kupunguza sauti kwenda kwenye menu unayoitaka. Kisha bonyeza cha kuwashia kuchagua menu yako.

Kama utakuwa ujaelewa basi tazama hii video ili kujua jinsi ya kuingia kwenye recovery. 



Kama unaswali lolote na unataka kusaidiwa kuhusiana na hii topic basi toa maoni yako chini.

2 comments:

  1. kaka niaje!!mie nina tatizo hapa!!nina galaxy note ii n7100 tatizo ni kwamba haiconnect internet

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabla ujafanya chochote nenda kwenye settings halafu nenda mobile networks kisha angalia kama kuna apn zozote. Kama zipo na simu yako bado haipati internet unaweza uka factory resert simu yako.

      Delete