Tuesday, June 10, 2014

( MAELEKEZO: ) JINSI YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY S3 IWE KAMA S4 NA NOTE 3


Kwa wale wadau wanatumia Samsung Galaxy S3 I9300, I9305 sasa wanaweza wakaifanya S3 ipate muonekano kama wa S4 na Note 3.

Nitatoa maelekezo jinsi ya kufanya ili uweze kupata muonekano wa S4 na Note 3 kwenye S3.
Picha zikionyesha Samsung Galaxy S3 ikiwa na muonekano wa S4/Note3








NOTE : VITU VYA KUZINGATIA

1) Hakikisha unafanya haya maelekezo kwenye simu aina ya samsung galaxy S3 I9300, I9305.
2)Hakikisha unautaalamu kidogo wa computer na elimu ya kuanzia form 4 na kuendelea.
3)MIMI SITAHUSIKA ENDAPO UTAHARIBU SIMU YAKO 
4)Hakikisha una internet connection ya kutosha kwa sababu utatakiwa kudownload vitu
5)Hakikisha memory card yako ina nafasi zaidi 2GB na kuendelea. 
6)Hakikisha simu yako ina charge ya kutosha (80% -100%) na battery yako ni nzuri.
7)Hakikisha simu yako ina  CLOCKWORKMOD RECOVERY kama cmw au twrp
8)Soma kwanza maelekezo yote na hakikisha unahelewa halafu ndio ujajaribu kwenye simu yako.


STEP 1:
Download RevolutionS4 rom. DOWNLOAD
Likisha malizika kudownload liweke kwenye memory card ya simu yako. Usiliweke ndani ya folder. 


STEP 2:
Zima simu yako (power off your device). Simu yako ikishazima kabisa basi bonyeza na kuvishikila vitufe hivi  (volume up+home+power) kwa sekunde kama 5 kisha achia cha power huku ukiwa umeendelea kuvishikilia (volume up+home)  mpaka utakapoona simu yako imekuletea custom recovery.

STEP 3:
Kwenye screen yako utaona kipengele cha kwanza kinasema install zip from sdcard. Kwa kutumia kitufe cha kupunguzia sauti bonyeza hadi utakapokifikia kipengele cha kwanza ambacho kinasema install zip from sdcard.
Kisha bonyeza kitufe cha kuwashia simu ili kuchagua hiyo menu.

STEP 4:
Simu yako itakuonyesha mafile yote yaliyomo kwenye memory card. Sasa wewe tafuta lile file uliloweka kwenye memory card (step1). Tumia cha kupunguza sauti au cha kuongeza ili kulichagua hulo file. Ukisha lifikia hilo file ambalo litakuwa linaitwa S4 Revolution v12 Christmas Version.zip bonyeza kitufe cha kuwashia simu. Kwa kutumia cha kupunguza sauti nenda hadi sehemu iliyoandikwa Yes kisha bonyeza cha kuwashia simu.

STEP 5:
Simu yako itaanza kuflash S4 Revolution Rom. Endapo kama simu yako itakwambia kama unataka kufuta kila kitu basi kubali na itaendelea ku-install mafile. Baada ya kumalizika basi washa simu yako na utapata muonekano wa S4 na Note 3 kwenye samsung galaxy s3.

Mpako hapo tumefikia mwisho kama wewe utakuwa na swali au ujaelewa basi toa comment chini na utajibiwa. Usiogope kuuliza. Kama umeshindwa kabisa sisi tunaweza kukusaidia kwa kiasi kisicho pungua Tsh 25000. Piga na +255716203029 au +255753618318.

No comments:

Post a Comment