Sunday, March 27, 2016

HIOS, MFUMO MPYA WA TECNO. KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA!

Tecno wameanzisha mfumo wao mpya ambao utakuwa unawekwa kwenye simu zao ili kuzifanya ziwe na muonekano mzuri kama ilivyo kwenye Samsung, Lg, Huawei etc. Tecno wanasema HIOS ni a brand tailored version optimizing user experience of Android Operating System. Ili kuelewa zaidi kitu Tecno wanachofanya ni kutengeneza muonekano wao wa kipee kama ilivyo Samsung-touchwiz, HTC-Sense, Huawei-Emotion Ui, Xiaomi-Miui.

Sasa tuangalie mambo yatakayo kuwepo kwenye HIOS ambayo itatolewa na Tecno mwezi wa April/2016. Tecno C8 ndio simu itakayo anza kutumia mfumo huu mpya. Unaweza tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka HIOS beta kwenye simu yako ya Tecno Camon C8
http://phonetricktz.blogspot.com/2016/03/jinsi-ya-ku-update-tecno-c8-ili-kutumia.html

MAMBO YATAKAYO KUWEPO KWENYE MFUMO MPYA WA TECNO "HIOS"

Quick Camera Activation

Hios inarahisisha kuwasha camera kwa haraka zaidi pale simu yako inapokuwa ipo kwenye lockscreen. Unachotakiwa kufanya ni kuipeleka ishara ya camera juu kisha camera itaanza kufanya kazi bila kuchelewa.

Easy Wallpaper Swipe

Hii ni njia itakayo kuwezesha kubadilisha picha ya wallpaper kwa haraka zaidi ili kuipa simu yako muonekano tofauti

Simple App Manager

Kama ilivyo kwenye simu nyingine za android, simple app manager itakuwezesha kuamisha apps na kuzipeleka kwenye home screen au popote pale unapotaka kupangilia apps zako

Personalized Photo Assistant

Kwa wale wanaopenda kupiga picha sasa Tecno wanawaletea Personalized Photo Assistant. Hii itakusaidia ku edit picha zako na kuzifanya ziwe nzuri na zenye mvuto.

Track Memory Usage

Kwenye Hios utaweza kuangalia jinsi apps zinavyotumia RAM ya simu yako. Hii ni jambo zuri maana utakuwa una uwezo wa kujua ni app ipi inatumia memory sana hivyo utakuwa na uwezo wa kufanya simu yako ifanye kazi kwa upesi zaidi kazi.

Hi Theme

Hi Theme ni njia itakayo kuwezesha kubadilisha muonekano mzima wa simu yako kwa hara zaidi. Hi Theme itakuwa ni sehemu ambayo itakuwa na themes mbalimbali ambazo utaweza kuzi download na kuziweka kwenye simu yako ili kupata muonekano wa kipekee.

Hi-Fonts

Hi-Fonts ni njia itakayo kuwezesha kubadili mfumo au muonekano wa maneno kwenye simu yako.

Pop Incoming Call

Pop Incoming Call ni mfumo ambao upo sanaa kwenye simu za samsung. Sasa Tecno wanaileta kwenye simu zao. Hii ina maanisha utaweza kuendelea na kitu unachofanya hata pale utakapo pigiwa simu

Hi Manager

Hi manager ni app ambayo itakusaidia kusafisha simu yako, kutoa apps ambazo zinasababisha simu yako isifanye kazi inavyopaswa.



Mpaka hapo tumefika mwisho na kama unataka kuendelea kupata habari kuhusiana na simu za tecno usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment