Monday, April 25, 2016

JINSI YA KU-UPDATE TECNO CAMON C8 KWENDA ANDROID 6.0 (MARSHMALLOW)

Miezi michache iliyopita, Tecno walitangaza mfumo mpya (HIOS) ambao utakuwa unatumika kwenye simu za Tecno. Tecno Camon C8 ni moja ya simu ambayo ipo kwenye mstari wa mbele kuanza kutumia mfumo huu mpya.

Leo nitatoa maelekezo jinsi ya kuweka mfuo wa hios pamoja na android 6.0 (marshmallow) kwenye Tecno Camon C8. Kwa wale ambao bado hawajui Hios ni nini basi tembelea link chini ili kufahau maana ya Hios na mambo ambayo yapo kwenye Hios
http://phonetricktz.blogspot.com/2016/03/hios-mfumo-mpya-wa-tecno-kipi.html

JINSI YA KU-UPDATE TECNO CAMON C8 KWENDA ANDROID 6.0 (MARSHMALLOW)

Vigezo na Masharti

  • 0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
  • 1: Hakikisha simu yako ni Tecno Camon C8
  • 2: Hakikisha simu yako ina charge kuanzia 70%
  • 3: Hakikisha simu yako ina Memory Card
  • 4: Soma maelekezo yote kwa makini kisha ndio ujaribu kwenye simu yako

NOTE

Tecno wanadai hii update kidogo ina matatizo. Watatoa update iliyo kamilika siku chache zijazo. Kama huwezi subiri endelea kusoma maelekezo chini kujua jinsi ya ku-update Tecno camon C8 na kuweka mfuo wa hios. Kwa wale wanaogopa kuaribu simu zao funga hii page ulale.

STEP 0

Download Tecno Camon C8 update kwa kutumia link chini.
https://mega.nz/#!UNwWTahA!y-z394qeOOxnoxrWgefBTe9vLqPjL_fTib6pGUMDMNw

STEP 1

Liweke hilo file ulilo download kwenye Step 0 ambalo linaitwa Tcard_update_20160415 kwenye memory card

STEP 2

Zima simu yako ya Tecno Camon C8. Kisha washa simu yako kwenye recovery mode. Ili kuwasha simu yako kwenye recovery mode unatakiwa ushikilie cha kuwashia na cha kuongeza sauti kwa pamoja na usiviachie mpaka simu yako itakapo onyesha logo ya Tecno kwenye display ndipo uviachie kama picha inavyo onekana chini

STEP 3

Subiri mpaka utakapo ona simu yako inafanana kama picha chini,

STEP 4

kisha bonyeza na kushikilia cha kuwashia kama sekunde mbili halafu bonyeza cha kuongezea sauti huku ukiwa umeshikila cha kuwashia na utapata muonekano kama picha chini. Kama ujapata muonekano kama picha chini rudia tena

STEP 5

Bonyeza cha kupunguza sauti mpaka utakofika kipengele kinachosema apply update from Sdcard kisha bonyeza cha kuwashia halafu bonyeza cha kupunguza sauti mpaka utakapofika kwenye lile file linaloitwa Tcard_update_20160415

STEP 6

Bonyeza cha kuwashia kisha subiri mpaka simu yako itakapo maliza ku update. Utaona simu yako imeandika update complete kama kwenye picha chini . Baada ya kumaliza simu yako itajiwasha yenyewe kama isipo jiwasha basi nenda kwenye kipengele kinachosema reboot system kisha bonyeza cha kuwashia.


Kumbuka simu yako itachelewa kuwa kwahiyo hakikisha unasubiri kama dakika 7-10.Mpaka hapo simu itakuwa imemaliza ku-update na utakuwa umefanikiwa kuweka Hios na android 6.0 kwenye Tecno Camon C8. Kama ungependa msaada kutoka kwetu unaweza wasilia nasi kwa kupitia whatsapp +255627732383.

Kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment