Saturday, April 30, 2016

JINSI YA KUONDOA ROOT NA KURUDISHIA ANDROID 5.0 KWENYE TECNO CAMON C8

Kwa wale ambao wame update simu zao za Tecno C8 kwenda android 6.0 au wale ambao wame root Tecno C8 na wangependa warudishe android 5.0 pamoja na kutoa root kwenye Tecno C8 au wale ambao wanapata matatizo kama simu kushindwa kuwaka na kuishia kwenye neno Tecno basi wanachotakiwa kufanya ni kufwatilizia maelekezo chini na wateweza kuiponyesha Tecno Camon C8.

JINSI YA KUONDOA ROOT NA KURUDISHIA ANDROID 5.0 KWENYE TECNO CAMON C8

Vigezo na Masharti

  • 0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
  • 1: Hakikisha simu yako ni Tecno Camon C8
  • 2: Hakikisha simu yako ina charge kuanzia 70%
  • 3: Hakikisha umeweka vcom driver kwenye computer yako
  • 4: Soma maelekezo yote kwa makini kisha ndio ujaribu kwenye simu yako

STEP 0

Hakikisha tayari umeweka vcom driver kwenye computer yako inayo tumia windows kama bado tembelea link chini kujia jinsi ya kuweka vcom driver kwenye computer yako
https://thebroodle.com/microsoft/windows/how-to-install-mtk65xx-preloader-usb-vcom-drivers-in-windows/

STEP 1

Download Tecno Camon C8 firmware kwa kutumia link chini
https://docs.google.com/uc?id=0B1ukKq9qHhpBVlRTM2tSS1JEUGM
au unaweza download kwa kutumia link chini
https://docs.google.com/uc?id=0B_pGM0vqvsl6Y21XM2J6QW9fWXM

STEP 2

Baada ya kumaliza ku download, lifungue (extract) hilo file ulilo download kwenye Step 1 na utapata mafile yanayo fanana kama kwenye picha chini

STEP 3

Download Sp Flash Tool na baada ya kumaliza ku download lifungue (extract) hilo file kwenye folder lolote kwenye computer yako. Ndani ya hilo folder double click file linaloitwa flashtool.exekama linavyo onekana kwenye picha chini

STEP 4

Nenda kwenye kipengele kinachosema Download kisha utapata muonekano kama picha chini. Kama hujapata muonekano kama picha chini rudia maelekezo tena

STEP 5

Bonyeza kipengele kinachosema Scatter-loading kama inavyo onekana kwenye picha chini

STEP 6

Computer itakwambia utafute file linaloitwa Android-Scatter. Kwa kutumia window mpya iliyofunguka kwenye computer yako, Nenda kwenye lile folder ambalo uli extract file ulilo download kwenye Step 2 kisha chagua file linaloitwa MT6735_Android_scatter.txt kisha bonyeza Open kama inavyo onekana kwenye picha chini

STEP 7

Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama kwenye picha chini. Kama ujapata muonekano kama kwenye picha chini, tafadhali rudia tena maelekezo.

STEP 8

Bonyeza kipengele kinachoitwa Download kama kwenye picha chini

STEP 9

Zima simu yako, kisha chomeka USB kwenye computer yako halafu chomeka kwenye simu yako. Kisha subiri mpaka utakapopata ujumbe unao sema OK kama kwenye picha chini



Kama ujapata muonekano kama picha juu basi hakikisha umefwatilizia maelekezo vizuri. Kama ukishindwa unaweza wasiliana nasi kupitia whatsapp number +255627732383.. Pia unaweza kutufwata kwenye instagram yetu kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment