Thursday, May 12, 2016

JINSI YA KU-UPDATE SAMSUNG GALAXY S5 KWENDA ANDROID 6.0.1

Samsung Galaxy S5 ni miongeni mwa smartphone ambazo zimepata android 6.0.1 (Marshmallow) na kama wewe ni mtumiaji wa Samsung Galaxy S5 sasa utaweza ku-update simu yako kutoka android 5 hadi kufikia android 6.0.1

JINSI YA KU-UPDATE SAMSUNG GALAXY S5 KWENDA ANDROID 6.0.1

Vigezo na Masharti

  • 0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
  • 1: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy S5
  • 2: Hakikisha simu yako ina charge kuanzia 70%
  • 3: Hakikisha ume install samsung drivers kwenye simu yako.

STEP 0

Download update kulingana na model ya simu yako. Inabidi ujiandikishe kwanza ndio utaweza ku download. Baada ya kumaliza ku-download lifungue hilo file kisha utapata file linalo ishia na maneno yanayo sema tar.md5

STEP 1

Download ODIN program kwa kutumia link chini kisha tengeneza folder kwenye desktop yako. Liweke hilo file ulilo download ndani ya folder kisha lifungue au extract
http://dl.sammobile.com/Odin3_v3.10.7.zip

STEP 2

Kwenye simu yako nenda kwenye settings kisha tafuta kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyo onekana chini. Kama hicho kipengele haukioni basi nenda kwenye about phone kisha shuka chini mpaka utakapoona kipengele kinachosema build number kisha kibonyeze haraka haraka kama mara saba kisha rudi tena kwenye setting na uangalie kama developer options imetokea

STEP 3

Fungua developer options kisha hakikisha umeiwasha (turn on) halafu umeweka tick ua umekiwasha kipengele kinachosema USB debugging kama picha inavyo onekana chini.

STEP 4

Zima simu yako kisha iwashe kwenye downloading mode. Kama hujui jinsi ya kuwasha simu kwenye downloading mode unachotakiwa kufanya ni zima (turn off) simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kupunguza sauti(vol down button)} na cha kuwashia (power button) mpaka simu itakapowaka kama picha inavyo onekana chini ndipo uachie vitufe vyote kwa pamoja.

STEP 5

Bonyeza kitufe cha kuongeza sauti kwenda kwenye Download Mode na utapata muonekano kama picha chini. Endapo una wasiwasi kwamba simu yako itaaribika au unaogopa na unataka simu yako irudi kama kawaida basi bonyeza kitufe cha kupunguza sauti au toa battery kisha rudishia kisha washa simu yako. Kama wewe hugopi na unataka kuendelea basi endelea kufwatilizia maelekezo

STEP 6

Rudi ndani ya lile folder ulilotengeneza kwenye Step 1, kisha double click ile program inayoitwa odin ambayo ulipata baada ya ku extract. Endapo upo sahihi utapata muonekano kama picha chini kwenye computer yako

STEP 7

Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy S5 halafu chomeka kwenye computer kisha kwenye program ya odin utaona kibox kinarangi kimeandikwa com(xx) na neno linalosema added kama picha chini

STEP 8

Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file linaloitwa tar.md5 ambalo uli download kwenye Step 0 kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.



Note
Hakikisha program yako ya odin ina fanana na picha juu kwa zaidi ya asilimia 98%. Haikisha vitiki kwenye program yako ya odin vina fanana na vyangu kisha subiri kama dakika 1

STEP 9

Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.

STEP 10

Simu yako itazima na kujiwasha. Chomoa USB yako kutoka kwenye computer. Subiri zaidi ya dakika 7 kwa maana simu yako itachelewa kuwaka. Baada ya simu yako kuwaka nenda kwenye about phone kisha tazama kama android yako imebadilika kutoka android 5.0 hadi kufikia 6.0.1

Mpaka hapo tumefikia mwisho, kama unataka kusaidiwa ku update Samsung Galaxy S5 au simu yoyote unaweza kutucheck kwenye kupitia whatsapp namba +255652732383.Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ambayo ni phonetricktz au unaweza like facebook yetu.

No comments:

Post a Comment