Thursday, October 30, 2014
GOOGLE FIT INAKUWEZESHA KUJUA JINSI YA KUWEKA MWILI WAKO IMARA
Mwaka 2014 tumeona big company kama Samsung wakianzisha S-HEALTH. Microsoft nao wakianzisha Microsoft Health huku Google nayo ikianzisha Google Fit.
S Health, Microsoft Health na Google Fit zote zina lengo moja la kukuwezesha kujua kiasi gani unapunguza vitu kama calories kwenye mwili wako kwa kutembea au kukimbia au hata kuendesha baiskeli.
Leo nitaiongelea sana Google Fit. Google Fit inakuwezesha kufanya mabadiliko makubwa kwenye afya yako na kukuweka imara. Kwa kutumia Google Fit unaweza kufwatilia mwili wako pale unapotembea, unapokimbia na pale pia unapoendesha baiskeli.
Google Fit pia inakuwezesha kufikia malengo yako ya kiafya ambayo unataka kufikia. Google Fit inapatika kwenye Google play store bure. Kwa wale wenye saa zinazotumia android pia watapata nafasi ya kujaribu Google Fit kwenye saa zao.
Picha chini ni baadhi ya screenshot zikionyesha jinsi google fit itakavyo kuwezesha kufikia malengo ya kiafya.
Ili kuweka Google Fit, simu yako inatakiwa iwe inatumia android 4.0 na kuendelea. Chini ya hapo utaweza kuweka Google Fit kwenye simu yako
For more info about android Please follow me on instagram #phonetricktz and dont forget to like my facebook
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment