Wengi wetu sio mara ya kwanza kusikia jina la Tecno kwenye masikio yetu. Tecno P5 ni smartphone ambayo inauwezo wa kutumia line mbili, RAM isiyopungua 512MB huku ikiwa inatumia android operation system (4.2.2)
Watu wengi wameniomba nitoe malekezo jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Tecno P5. Kwa kifupi custom recovery ni application inayokuwezesha kuflash rom mbali mbali kwenye simu yako pia inakuwezesha kufanya backup ya simu yako na ku restore backup.
Leo nitatoa malekezo jinsi ya kuweka clockworkmode recovery kwenye Tecno P5.
VIGEZO NA MASHARTI
- Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
- Computer Knowledge is recommended.
JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY (CWM) KWENYE TECNO P5
STEP 0
Hakikisha simu yako ni Tecno P5. Tafashali usijaribu kwenye simu ambayo sio Tecno P5
STEP 1
Hakikisha Tecno P5 yako tayari imekuwa rooted. Kama bado tembelea link chini ili uweze ku root Tecno p5.
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/11/maelekezo-jinsi-ya-ku-root-tecno-p5.html
STEP 2
Download Recovery Tools app kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu yako ya Tecno P5
https://www.dropbox.com/s/prnivfy87dt5pky/Recovery-Tools.apk?dl=0
STEP 3
Download TECNO P5 RECOVERY.img kisha liweke hilo file kwenye memory ya simu
https://www.dropbox.com/s/dj3jk88np4zu6ze/TECNO-P5_RECOVERY.img?dl=0
STEP 4
Fungua Recovery Tools application. Hakikisha unabonyeza kipengele cha GRANT kwenye simu yako na utapata muonekano kama kwenye picha ya pili chini
STEP 5
Nenda kwenye kipengele cha Flash Recovery kisha chagua lile file ambalo ume download kwenye step 3 (TECNO P5 RECOVERY.img) ambalo uliliweka kwenye phone memory kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa "yes please"
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye Tecno P5. Ili kuhakikisha zima simu yako kisha subiri kama sekunde 5 kisha bonyeza cha kuwashia na cha kuongeza sauti kwa wakati mmoja kisha vishikilie mpaka utakapoona picha kama hiyo hapo chini
No comments:
Post a Comment