Tuesday, December 22, 2015

TECNO CAMON C8. KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA!

Tecno C8 sio simu ya kuibeza au kuichukulia poa kama ilivyo zoeleka kwa matoleo mengine ya Tecno. Tecno kiukweli wameanza kufanya vizuri sana Mwaka 2015 kwa kutoa simu ambazo zimetokea kupendwa na watu sana.

Miezi michache iliyopita Tecno waliitambulisha Tecno Cannon C8 ikiwa imebeba mambo mengi mazuri kama kioo chenye ukubwa wa 5.5 inches, resolution ya 720 X 1280 pixes High Definition.



Kwa upande wa camera, Tecno C8 haijawangusha watumiaji ikiwa na camera ya nyuma yenye uwezo wa 13 Megapixels pamoja na LED FLash na Auto focus. Camera ya mbele nayo imetushangaza kwa kuwa na Flash na uwezo wa 5 Megapixels. Kwa wale wanaopenda mambo ya Selfie watajisikia wapo nyumbani kwa kuweza kupiga Selfies hata kwenye giza au sehemu yenye mwanga hafifu.



Tecno C8 ina kuhakikishia speed na ufanisi mkubwa kwa kuwa na RAM ya 1GB, processor yenye speed kiasi cha 1.3GHz quad-core . 16GB ni nafasi ya ndani ambayo ita kusaidia kuweka picha, video, apps pamoja na document zako. Endapo kama utakuwa hauridhiki na 16GB basi utaweza kuweka memory card yenye ukubwa wowote mpaka 32GB.



Kwa upande wa software, Tecno C8 inatumia android 5.0.2 lollipop ikiwa inafanana sana stock android. Kwa maelezo zaidi tazama jedwali chini kuendelea kujua mambo mazuri mengi yaliyomo kwenye Tecno C8

Bei Kuanzia Tsh 300,000
Aina ya Simu Phablet
OS Android 5.0.2 (lollipop)
Processor 1.3 GHz Quad-core Cortex A53,
MediaTek MT6735 chipset (64-bit)
RAM 1GB
GPU Mali-T720
Internal storage 16GB
External storage Micro SD, up to 32GB
Ukubwa wa kioo 5.5 inches
Resolution 1280 X 720 pixels
Pixel density 267 ppi
SIM Type SIM1: Mini-SIM, SIM2: Micro-SIM
Network Support 2G - Yes
3G - Yes
4G - No
Internet & Connectivity GPRS - Yes
EDGE - Yes
3G/WCDMA/HSPA - Yes
HSPA+ - Yes
4G LTE - Yes
WLAN - Yes(Wi-Fi 802.11 b/g/n)
Wi-Fi Hotspot - Yes
Bluetooth - Yes
NFC - No
USB Port - Yes, microUSB 2.0
Camera Camera ya Nyuma - 13 MP, HD Video,dual-LED Flash
Camera ya Mbele - 5MP Camera, LED Flash
Burudani Music Player-Yes, mp3, WAV, FLAC, eACC+
Video Player: Yes, MPEG4, H.263, H.264, XviD
FM Radio: Yes
Battery 3000 mAh Li-ion Battery


Endapo ungependa kununua Tecno C8 kwa bei nzuri unaweza wasiliana nasi kupitia namba +255716203029. Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment