Saturday, November 28, 2015

JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S5 (SM-G900F)

Samsung Galaxy S5 ni smartphone ambayo wengi wetu hatuwezi kuisahau mapema kutokana na uwezo wake wa kutoingia maji. Licha ya kuwa na sifa nyingi Samsung Galaxy S5 haikuweza kupata soko kubwa kama ilivyokuwa kwa wadogo zake ambao ni S3 na S4.

Leo tutaongelea jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S5. Custom recovery ni njia inayokuwezesha kuweka custom rom, mods, ku-backup na ku-restore simu yako. Pengine utakuwa unajiuliza kwa nini tuweke custom recovery? Ina maana simu za android huwa hazina custom recovery?

Jibu ni kwamba simu za android huwa zinakuja na recovery yake lakini hii recovery haina uwezo wa kukusaidia kuweka custom recovery au ku-backup na ku-restore simu yako. Ndio maana wengi wetu huwa tunaweka custom recovery maana inafanya uweze kuitumia simu yako kikamilifu.

Ili kujua recovery ambayo imekuja na simu yako unachotakiwa kufanya ni kuzima simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuwashia (power button) na cha kuongeza sauti(vol up button)} mpaka simu itakopo onyesha logo ya Samsung kisha viachie vitufe kwa pamoja. Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama picha chini.



Kama ndio mara yako ya kwanza kufanya hivyo na hujui jinsi ya kurudisha simu kama ilivyokuwa basi chakufanya toa battery kisha rudishia kisha washa simu yako kawaida. Bila kuongea sana twende tukaangalie jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S5.

JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S5 (SM-G900F)


Vigezo na Masharti

  • 1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.

  • 2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer

  • 3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S5 (SM-G900F)

  • 4: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window


STEP 0

Download Samsung usb drivers kwa kutumia link chini kisha install kwenye computer yako
http://www.devfiles.co/download/AbRa7wHc/SAMSUNG_USB_Driver_for_Mobile_Phones.exe

STEP 1

Download ODIN program kwa kutumia link chini kisha tengeneza folder kwenye desktop yako. Liweke hilo file ulilo download ndani ya folder
http://dl.sammobile.com/Odin3_v3.10.7.zip

STEP 2

Download TWRP recovery kwa kutumia link chini na mara baada ya kumaliza ku-download liweke hilo file ndani ya folder ulilotengeza kwenye Step 1.
https://mega.nz/#!Ac52QQhR

STEP 3

Rudi kwenye lile folder ulilotengeneza kwenye Step 1, Extract ile program (odin3_v3.10.7) uliyo donwload kwenye Step 1 humo humo ndani ya folder.

STEP 4

Kwenye simu yako nenda kwenye settings kisha tafuta kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyo onekana chini. Kama hicho kipengele haukioni basi nenda kwenye about phone kisha shuka chini mpaka utakapoona kipengele kinachosema build number kisha kibonyeze haraka haraka kama mara saba kisha rudi tena kwenye setting na uangalie kama developer options imetokea

STEP 5

Fungua developer options kisha hakikisha umeiwasha (turn on) halafu umeweka tick ua umekiwasha kipengele kinachosema USB debugging kama picha inavyo onekana chini.

STEP 6

Zima simu yako kisha iwashe kwenye Download Mode. Kama hujui jinsi ya kuwasha simu yako kwenye Download Mode unachotakiwa kufanya ni zima (turn off) simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuwashia (power button) na cha kupunguza sauti(vol down button)} mpaka simu itakapowaka kama picha inavyo onekana chini ndipo uachie vitufe vyote kwa pamoja.

STEP 7

Bonyeza kitufe cha kuongeza sauti kwenda kwenye Download Mode na utapata muonekano kama picha chini. Endapo una wasiwasi kwamba simu yako itaaribika au unaogopa na unataka simu yako irudi kama kawaida basi bonyeza kitufe cha kupunguza sauti au toa battery kisha rudishia kisha washa simu yako. Kama wewe hugopi na unataka kuendelea basi endelea kufwatilizia maelekezo

STEP 8

Rudi ndani ya lile folder ulilotengeneza kwenye Step 1, kisha double click ile program inayoitwa odin ambayo ulipata baada ya ku extract. Endapo upo sahihi utapata muonekano kama picha chini kwenye computer yako

STEP 9

Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy S5(SM-G900F) halafu chomeka kwenye computer kisha kwenye program ya odin utaona kibox kinarangi kimeandikwa com(xx) na neno linalosema added kama picha chini

STEP 10

Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file linaloitwa openrecovery-twrp-2.8.5.0-gt-klte ambalo uli download kwenye Step 2 kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.



Note
Hakikisha program yako ya odin ina fanana na picha juu kwa zaidi ya asilimia 98%. Haikisha vitiki kwenye program yako ya odin vina fanana na vyangu

STEP 11

Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.

STEP 12

Chomoa USB yako kwenye computer. Ili kuona recovery mpya iliyopo kwenye simu yako basi rudia kama ulivyofanya pale ulipokuwa unataka kuangalia recovery ambayo imekuja na simu yako. Recovery mpya itakuwa na muonekano kama picha chini

Mpaka hapo tumefikia mwisho, kama unataka kusaidiwa kuwekewa custom recovery kwenye Galaxy S5 au simu yoyote unaweza kutucheck kwenye Viber au Tango kupitia namba +255788127975

Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ambayo ni phonetricktz au unaweza like facebook yetu.

3 comments:

  1. Msaada jinsi ya kuweka custom recovery kwenye tecno h6

    ReplyDelete
  2. Msaada jinsi ya kuweka custom recovery kwenye tecno h6

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umejaribu kutumia flashfy au piga namba 0753877552 kwa maelekezo zaidi

      Delete