Tuesday, December 1, 2015

JINSI YA KUWEKA ANDROID 5.1.1 KWENYE SAMSUNG GALAXY S5 (SM-G900F)

Samsung Galaxy S5 kwa sasa inatumia android 5.0 na kupelekea kupitwa hata na mdogo wake S4 ambaye anatumia android 5.0.2. Hii ni aibu kubwa kwa watumiaji wa Galaxy S5 ambayo ingepaswa iwe inatumia hata android 6.0 (marshmallow).

Leo tutajifunza jinsi ya kuweka android 5.1.1 kwenye Samsung Galaxy S5 (SM-G900F) na kuifanya ifanane na Galaxy Note 5. Tutatumia custom rom inayoitwa S5 Revolution ambayo kiukweli ni moja ya custom rom bora ya S5 ikiwa ina mambo mengi ambayo yataifanya Galaxy S5 yako iwe kama Note 5 na S6 edge.

JINSI YA KUWEKA ANDROID 5.1.1 KWENYE SAMSUNG GALAXY S5 (SM-G900F)

Vigezo na Masharti

  • 1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.

  • 2: Soma maelekezo kwa maakini kabla ujajaribu kwenye simu yako

  • 3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S5 (SM-G900F)

  • 4: Hakikisha simu yako ina charge kuanzia 75%

  • 5: Hakikisha memory card yako au simu yako ina nafasi zaidi ya 8GB

STEP 0

Hakikisha tayari umeweka custom recovery kwenye simu yako ya Galaxy S5. Kama bado ujaweka custom recovery tembelea link chini ili ujue jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Galaxy S5
http://phonetricktz.blogspot.com/2015/11/jinsi-ya-kuweka-custom-recovery-kwenye.html

STEP 1

Download S5 Revolution rom kwa kutumia link chini kisha liweke hiko file kama lilivyo kwenye memory card ya simu yako.
https://mega.nz/#!XFpTiIrb!y4E9oGZoGQkX4bF4Hf92OueKGIR95raMGUFZ56OgwzU

STEP 2

Washa simu yako kwenye Recovery Mode. Kama utakuwa umeweka TWRP Recovery basi utakuwa na muonekano kama picha chini

STEP 3

Ukiwa kwenye Recovery Mode bonyeza kipengele kinachosema backup. Baada ya hapo hakikisha una weka tick kwenye vipengele vyote (system, data, boot, cache, modem, efs) kisha chini utaona umeambiwa swipe to backup. Subiri mpaka backup imalizike na utaona ujume umekwambia backup complete

STEP 4

Rudi tena kwenye menu kuu ya recovery utaona kipengele kinachosema wipe. Bonyeza kipengele cha wipe kisha chini utaona umeambiwa swipe to wipe. Hakikisha una swipe ili ufute kila kitu kwenye simu yako iwe tayari kwa ajili ya kuweka S5 Revolution rom.

STEP 5

Rudi tena kwenye menu kuu ya recovery utaona kipengele kinachosema install. Bonyeza kipengele cha install halafu tafuta lile file ambalo uli download kwenye Step 1 na ukaliweka kwenye memory card. Kama ujui jinsi ya kubadilisha ili recovery yako iweze kusoma memory card yako usipate shida ukiwa hapo hapo kwenye hicho kipengele cha install juu kabisa ukibonyeza utaona umepewa option mbili ambazo ni internal storage na external storage ambayo ndio memory card yako. sasa chagua external storage kisha litazame tena lile file ulilodownload kwenye step 1. Bonyeza hilo file kisha chini utaona umeambiwa swipe to install. Hakikisha una swipe kisha subiri mpaka simu ikupe ujumbe kwamba install complete.

STEP 6

Rudi tena kwenye menu kuu ya recovery utaona kipengele kinachosema reboot. Kibonyeze hicho kipengele kisha bonyeza kipengele kinachosema system. Simu yako itazima na itajiwasha yenyewe. Simu yako itachukua mdaa kuwaka kama dakika 11.

STEP 7

Endapo simu yako ikiwaka ukienda kwenye about phone basi utakuwa na muonekano kama picha chini



Mpaka hapo tumefikia mwisho, kama unataka kusaidiwa kuwekewa custom recovery au custom rom kwenye Galaxy S5 au simu yoyote unaweza kutucheck kwenye Viber facebook messenger au Tango kupitia namba +255788127975

Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ambayo ni phonetricktz au unaweza like facebook yetu.

No comments:

Post a Comment