Saturday, March 12, 2016

ANDROID N: TOLEO JIPYA LA ANDROID BAADA YA MARSHMALLOW

Kila mwaka huwa tunapata mambo mengi sana kutoka Google na moja wapo ni toleo jipya la android. Kama ilivyo kawaida mwaka huu google wanatuletea toleo jipya kabisa la android ambalo litaitwa Android N

Katika hili tolea jipya la android (Android N) mambo mengi sana yame boreshwa pia kuna mambo mengine mapya yameongezwa kwenye andorid. Bila kuongea sana embu tuangalie mambo mapya yalioyo ongezwa kwenye Android N

SETTINGS

Kwenye Android N, Settings imeboreshwa na sasa utaweza kupata information kidogo kuhusu kila kipengele kilichopo kwenye settings. Unaweza tazama picha chili ili kuelewa zaidi. Mfano ukitazama kwenye picha chini kwenye kipengele cha storage utaona simu yako inakwambia kiasi cha storage(nafasi) ulichotumia bila hata kuingia ndani kama ilivyo kwenye mifumo ya android iliyopita. Pia ukitazama kwenye kipengele cha battery utaona chini yake una ambiwa kilichobaki.



SIDEBAR SETTINGS

Sidebar Settings ni kipengele kipya ambacho kitakuwepo kwenye Android N. Kwa mfano ukiwa ndani ya kipengele chochote cha settings utakapo swipe screen yako kwenda kulia basi utapata sidebar settings ambayo utaweza kwenda kwenye kipengele kingine cha settings bila kurudi nyuma. Lengo kubwa la Sidebar Settings ni kumuwezesha mtumiaji wa android kufanya mambo kwa haraka zaidi bila kupoteza muda.



NOTIFICATION PANEL

Notification Panel ni ile ambayo huwa unavuta screen yako kutoka juu kuelekea chini ili uweze kuona taarifa zozote mpya amabazo umezipa kutoka kwenye social networks, emails au hata remainder kutoka kwenye application tofauti tofauti. Kwenye Android N, Notification panel imepata muonekano mpya kabisa. Kila notification ambayo utaipata itakuja na maelezo yake ya kutosha tofauti na ilivyo kuwa kwenye matoleo ya android yalitopita



MULTI-TASKING

Kwa ambao hawajua Multitasking ni uwezo wa kufanya vitu viwili kwa wakati mmmoja. Multitasking sio kitu kipya kwenye simu kama Samsung au LG. Sasa google wameamua kuitambulisha multitasking rasmi kwenye tolea jipya la Android N. Kwenye Android N utaweza kuigawanya screen yako mara mbili na kila screen utaweka app unayotaka na screen nyingine utaweka app nyingine unayotaka na zote utaweza kuzitumia kwa wakati mmoja.



NIGHT MODE

Night mode ni kitu kipya kabisa kuletwa kwenye android. Kwa wale ambao walikuwa wanatumia custom rom mambo kama Night Mode sio jambo jipya kwao. Night mode ni njia ya kukuweza kuweza kutumia simu yako hata kwenye sehemu ambazo zina mwanga mchache. Pia Night Mode ni nzuri kwa kukupunguzia matumizi mabaya ya battery.



Tazama video chini kuona mambo yote yaliongezwa kwenye Android N



Baada ya kuona mambo mapya ambayo yatakuwepo kwenye toleo jipya la Android, sasa swali linakuja wewe mtumiaji wa android unawezaje kuweka Android N kwenye simu yako? Jibu ni kwamba kama wewe unatumia simu kama Nexus 6p au Nexus 5x basi utaweza kuanza kutumia Android N baada ya kujisajili.

Endapo wewe utataka kuanza kutumia Android N kwenye simu yako basi fwatilizia maelekezo yafuatayo?

STEP 0

Login kwenye site Android N beta kwa kutumia account yako ya Gmail. Tembelea Android N beta website kwa kutumia link chini
https://www.google.com/android/beta

STEP 1

Chagua simu ambayo unayotaka kuweka Android N. Hakikisha simu yako ni moja kati ya hizi zifuatazo
  • Nexus 5X
  • Nexus 6
  • Nexus 6P
  • Nexus 9 Wi-Fi
  • Nexus 9 LTE
  • Pixel C
  • Nexus Player
  • General Mobile 4G (Android One)

STEP 2

Bonyeza Enroll Device kisha agree to the Terms of the Agreement. Kisha subiri ndani ya masaa 24 na utapata ujumbe jinsi ya kudownload android n na kuiweka kwenye simu yako.

Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu basi usiache kutufwata kwenye instagram kwa kutumia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment